• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe |
Arusha District Council
Arusha District Council

Serikali ya jamuhuri ya Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili Makuu
    • Mikkati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara na Vitengo
      • Utawala na Utumishi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Fadha na Biashara
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliji
      • Ardhi na Maliasili
      • Maji
      • Works
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo na Umwagiliaji na Ushirika
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Internal Audit
      • Nyuki
      • Uchaguzi
      • UKIMWI/ AIDS
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Livestock
    • Wadau wa Maendeleo
  • Huduma Zetu
    • Health
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Utawala Fedha na Mipango
      • Elimu Afya na Maji
      • Kudhibiti UKIMWI
      • Maadili ya Madiwani
      • Uchumi Ujenzi na Mazingira
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Vikao vya Timu ya Uendeshji ya Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mktaba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa UMMA
    • Video za Shoghuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

SERIKALI YABABAINI MAPUNGUFU MAABARA YA TAIFA - RIPOTI YA UCHUNGUZI

Posted on: May 23rd, 2020

Na WAMJW – Dar es Salaam

23/05/2020

Serikali imetoa ripoti ya uchunguzi wa Maabara ya Taifa ya Afya ya Jamii iliyoko ofisi za Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binaadam (NIMR) jijini Dar es Salaam na kubaini mapungufu mbalimbali ya kiutendaji yaliyokuwepo katika maabara hiyo.

Akiwasilisha taarifa ya kamati hiyo leo jijini Dar es Salaam, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mheshimiwa Ummy Mwalimu ametaja mapungufu yaliyobainishwa na kamati hiyo kuwa moja kati ya mashine za kupima sampuli za COVID-19 ilikuwa na hitilafu bila uongozi wa maabara kuchukua hatua za kuifanyia matengenezo.

Taarifa hiyo pia imebaini kuwepo kwa upungufu katika mfumo wa kimuundo, kiutendaji na uendeshaji wa kitaaluma katika upimaji wa vipimo, uhakiki wa ubora wa majibu na udhaifu katika uhifadhi wa vipimo vya COVID-19.  

Waziri Ummy amesema kamati hiyo pia imetaja kuwepo kwa upungufu wa wataalamu wenye sifa za mafunzo ya “Biotechnology & molecular Biology” katika sekta ya Afya ikiwemo katika Maabara ya Taifa ya Afya ya Jamii.

Kufuatia taarifa ya kamati ya uchunguzi wa Maabara ya Taifa ya Afya ya Jamii kuhusu upimaji wa sampuli za ugonjwa wa COVID- 19, Wizara ya Afya imechukua hatua ya kuhamisha shughuli za upimaji wa COVID – 19 kutoka kwenye maabara iliyoko NIMR na  kuanza kutumika kwa mashine nyingine za maabara mpya iliyopo Mabibo, Dar es salaam.

“Kuanzia sasa shughuli zote za upimaji wa maabara ya taifa ya afya  ya  jamii zitafanyika katika maabara mpya ya mabibo yenye vifaa vya kisasa vyenye ubora na uwezo wa kupima sampuli 1,800 ndani ya masaa 24” amesisitiza Waziri Ummy.

Amesema maabara iliyokuwa inatumika awali na kukutwa na mapungufu ilikuwa na uwezo wa kupima sampuli 300 kwa masaa 24 na ilianzishwa mwaka 1968 katika ofisi za Taasisi ya Utafiti wa Magonjwa ya Binaadam (NIMR), mtaa wa Obama kati kati ya jiji la Dar es Salaam zitaendelea kupima magonjwa mengine.

“hivi sasa Upimaji wa Sampuli zote za COVID-19 umehamishiwa kwenye Maabara hii ya Mabibo, Dar es Salaam ambayo kuanzia sasa ndiyo itakuwa Maabara ya Taifa ya Afya ya Jamii. Maabara hii ambayo ujenzi wake umekamilika mwezi huu ina miundombinu inayojitosheleza, mashine za kisasa zinazoweza kupima sampuli nyingi na kutoa majibu ya uhakika na kwa haraka” amesema Waziri Ummy.

Aidha, Wizara imeshaandaa wataalam zaidi wenye sifa na vigezo kwa ajili ya Maabara hiyo na imeanza kurekebisha mfumo wa utawala, utendaji na kitaaluma ndani ya Maabara ya Taifa.

Waziri Ummy Mwalimu aliunda Kamati ya wataalam iliyoanza kazi rasmi tarehe 6, Mei, 2020 ya kuchunguza mwenendo wa maabara ya taifa ya afya ya jamii ikiwa ni pamoja na kuangalia mfumo mzima wa ukusanyaji na upimaji wa sampuli za COVID – 19.

Kamati hiyo iliundwa kufuatia mashaka yaliyoelezwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt John Pombe Magufuli kuhusu usahihi wa vipimo vya COVID – 1.

Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Abel Makubi ametoa mwongozo wa kusaidia jamii kushiriki katika ibada ya shukrani na sala ya Eid El Fitr kwa hali ya usalama ili kuepusha kuongezeka kwa maambukizi ya virusi vya corona.

Akizungumza jijini Dar es Salaam leo, Prof. Makubi amewataka  wananchi kuchukua tahadhari katika siku tatu ambazo nchi itaingia katika maombi maalum ya kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa ajili ya kupungua kwa maambukizi ya virusi ugonjwa wa Corona.

“ Ni muhimu wananchi wakasherehekea salama kwa kuchukuwa  tahadhari kwani ugonjwa huo bado upo” Amesisitiza Mganga Mkuu wa Serikali.

Katika kufanikisha uwepo wa mazingira salama wakati wa shukrani na sala ,Viongozi wa Mitaa, Viongozi wa Afya na uongozi wa maeneo yote ya Ibada na misikitini wanapaswa kuhakikisha uwepo wa vifaa vya kunawia mikono, maji tiririka na sabuni au vitakasa mikono kwa ajili ya usafi binafsi wa waumini wote katika maeneo ya kuingilia .

Aidha, Prof. Makubi ameshauri sehemu za kufanyia ibada ziwe na nafasi ya viti kupangwa zaidi ya mita moja kwa wale wanaokaa au kusimama na wananchi wote wanapokwenda kushiriki au kutembelea maeneo ya Ibada/Sala wanashauriwa watumie barakoa za vitambaa ambazo kwa sasa zipo kwa wingi na zinatengenezwa hapa nchini na wananchi wenyewe.

Amewataka wananchi kuepuka mikusanyiko na kuhakikisha wanakaa umbali usipoungua mita moja kati ya mtu na mtu wakati wote wa shukrani na wakati wa shukrani waendesha ibada/sala wawakumbushe wananchi mara kwa mara kuzingatia taratibu za kujikinga na maambukizi kama inavyoelekezwa na wataalamu wa afya

Mganga Mkuu wa Serikali amewakumbusha Wamiliki wa vyombo vya usafiri wa umma kuzingatia maagizo ya Serikali ya kutosimamisha abiria kwenye mabasi, na vilevile wahudumu wote wawe wamevaa barakoa za vitambaa.

MWISHO






Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA MKATABA ENABOISHU FM - ARUSHA DC May 26, 2025
  • ORODHA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO 2023 ARUSHA DC June 11, 2023
  • ZIARA YA WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS TAMISEMI, MHE. MOHAMED O. MCHENGERWA 17 SEPTEMBA 2024 September 13, 2024
  • MTIHANI WA DARASA LA SABA 11-12/09/2024 September 09, 2024
  • Tazama zote

Habari mpya

  • VIONGOZI WA DINI WAPEWA ELIMU YA CHAKULA BORA

    May 28, 2025
  • VIONGOZI WA DINI WAPEWA ELIMU YA AFYA YA MAMA NA MTOTO

    May 27, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA MKATABA

    May 26, 2025
  • RC MAKONDA ATEMBELEA NA KUKAGUA MRADI WA UJENZI WA MAHAKAMA YA AFRIKA ARUSHA

    May 25, 2025
  • Tazama zote

Video

Video zaidi

Viunganishi vinavyoingiliana

  • Leseni ya vileo
  • Fomu ya ukaguzi

Viunganishi vinavyohusiana

  • Tovuti kuu ya serikali
  • Tamisemi
  • Utumishi portal
  • Wakala wa serikali mtandao
  • Mkoa wa arusha
  • ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Sekei Road

    Anuani ya posta: 2330 Arusha

    Simu : +255 027 2502737

    Simu: 073 65000476

    Barua pepe: ded@arushadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.