Shule ya sekondari Mwandat imeibuka kidedea ikipeperusha bendera yake ya kitaaluma kwa kushika nafasi ya kwanza kati ya shule 10 za halmashauri ya Arusha kwa matokeo ya Mtihani wa Taifa wa Kidato cha sita mwaka 2023.
Katika matokeo hayo, halmashauri ya Arusha imepata ufaulu wa asilimia 100 kwa wanafunzi 851 waliofanya mtihani wa kuhitimu kidato cha sita mwaka 2023.
Kati ya wanafunzi hao 851, wanafunzi 517 wamepata daraja la I, wanafunzi 265 wakipata daraja la II, wanafunzi 68 wakipata daraja la III na mwanafunzi 1 tuu akipata daraja la IV kukiwa hakuna daraja 0.
Uongozi wa halmashauri ya Arusha unawapongeza wanafunzi, wazazi, walimu, maafisa elimu wote wakiongozwa na Mkuu wa Idara ya Elimu Sekondari kwa umoja wao kufanikisha ufaulu wa hali ya juu wa wanafunzi wote wa kidato cha sita mwaka 2023.
ARUSHA DC BILA SIFURI INAWEZEKANA
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.