Na. Elinipa Lupembe
Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa wilaya ya Arumeru, imekabidhi miongozo iliyoandaliwa na TAKUKURU Taifa, kwa Uongozi wa Wilaya ya Arumeru na Kamishna wa Skauti wilaya ya Arumeru, miongozo ambayo ni mkakati wa kuzuia na kupambana na Rushwa nchini kwa kuwashirikisha Vijana wa Skauti.
Akizungumza wakati wa hafla fupi ya makabidhiano iliyofanyika kwenye ofisi ya mkuu wa wilaya ya Arumeru, mapema wiki hii, Mkuu wa TAKUKURU wilaya ya Arumeru, Deo Mtui amesema kuwa, TAKUKURU imeandaa Mwongozo uliowashirikisha Skauti wenye kauli mbiu ya TAKUSKA, ambao ni mkakati wa kuzia na Kupambana na Rushwa nchini.
Aidha Kamanda Mtui ameeleza kuwa, lengo kuu la kuungana kwa TAKUKURU NA SKAUTI na kutengeneza TAKUSKA ambayo itahakikisha vijana wote nchini, hususani wanafunzi wa shule za Msingi na Sekondari, wanapata fursa ya kufundishwa Uzalendo,Uwajibikaji na Uadilifu, wakiwa shuleni, wangali bado vijana wadogo.
"TAKUKURU wilaya ya Aruemru imesimamia uanzishwaji wa Vilabu vya Kupinga ma kupambana na Rushwa kwenye shuke za msingi na sekondari za halmashauri ya Arusha na Meru, kupitia vilabu hiyo vya wapinga Rushwa shuleni, vijana hao watafundishwa maadili na uzalendo kupitia Miongozo hiyo ya TAKUSKA tuliyoikabidhi leo kwa Mkuu wa Wilaya ambaye ni Mwenyekiti wa Skauti wa Wilaya pamoja na Kamishna wa Skauti wa wilaya ili vikatumike kwa manufaa ya vijana na Taifa letu" amesisitiza Kiongozi hiyo wa TAKUKURU.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Mhandisi Richard Ruyango, licha ya kuipongeza TAKUKURU na SKAUTI kwa kunganisha nguvu katika harakati za Kuzuia na Kupambana Rushwa nchini, na kuongeza kuwa anaamini kupitia miongozo ya TAKUSKA, itawajengea uwezo vijana walioko shuleni na kuwaandaa vema kuwa vijana wenye maadili, wawajibikaji, na wazalendo katika kuitumikia nchi yao.
Hata hivyo mkuu huyo wa wilaya amewataka Wakuu wa Idara za Elimu Msingi na sekondari katika halmashauri za Arusha na Meru, kuafanya utaratibu wa kukitafutia Chama Cha SKAUTI kwenye amjengo ya serikali ili waweze kufanya kaiz kwa ufanisi zaidi.
Naye Kamishina wa SKAUTI Wilaya ya Arumeru, Justice Yona ametoa rai kwa Mkuu wa Wilaya na Viongozi wote walioshiriki ambao ni Wakuu wa Idara za Elimu Msingi na SEKONDARI wa Halmashauri zote mbili za Meru na Arusha DC kuandaa kikao ambacho yeye Kamishna wa Skauti, atakuja kuwaelimisha wataalamu wote juu ya SKAUTI Kwa kushirikiana na TAKUKURU wilaya ya ARUMERU
Awali TAKUSKA ilizinduliwa rasmi tarehe 02/03/2020 na aliyekuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya TANZANIA ambaye Kwa sasa ndiye Rais wa Jamhuri ya Muungano wa TANZANIA Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, ambaye aliwakilishwa na aliyekuwa Mheshimiwa, Waziri wa Utawala Bora George Huruma Mkuchika jijini DODOMA na wilaya ya Arumeru imeanza utekelezajiw ake katika halmashauri zake mbili za Arusha na Meru.
ARUMERU
kaziInaendelea✍✍✍
Mkuu wa TAKUKURU wilaya ya Aruemru Deo Mtui ( wa kwanza Kushoto) akimkabidhi mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Mhandisi Richard Ruyango, miongozo wa TAKUSKA utakaotumiksa kuwafundisha vijana kupinga na kupambana na rushwa, pamoja na kuwajengea uwezo wa kuwa wazalendo, waadilifu na wawajibikaji.
Mkuu wa TAKUKURU wilaya ya Arumeru, Deo Mtui akiwakabidhi miongozo wa TAKUSKA , mkuu wa wilaya ya Arumeru, Mhandisi Richard Ruyango na Kamishna wa Skauti Arumeru, utakaotumiksa kuwafundisha vijana kupinga na kupambana na rushwa, pamoja na kuwajengea uwezo wa kuwa wazalendo, waadilifu na wawajibikaji.
Picha pamoja iliyojumisha Mkuu wa wilaya ya Arumwru, Vijana wa SKAUTI Wilaya ya ARUMERU, Wakuu wa Idara za Elimu Msingi, Sekondari na Maafisa Taaluma wa Halmashauri za Arusha na Meru.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.