Na. Elinipa Lupembe.
Timu ya mpira wa pete halmashauri ya Arusha, wamemkabidhi mkurugenzi mtendaji wa halmashauri hiyo kikombe cha ushindi, baada ya kushinda katika mashindano ya kombe la Magonjwa yasiyo yankuambukizwa yaliyofanyika mkoani Arusha, kwa kuandaliwa ma Wizara ya Afya.
Akipokea Kikombe hicho ofisini wkake, mkurugenzi mtendaji halmasahsuri ya Arusha, Seleman Msumi, licha ya kuwapongeza wachezajinhao kwa ushindi huo wa kishindo, ulioiletea sifa halmashauri ya Arusha, amewataka watumishi wa halmashauri hiyo, kutenga muda baada ya saa za kazi, kushiriki michezo kwa kuwa michezo inajenga afya na inaboresha uwezo wa kufanyakazi.
Mkurugenzi Msumi ameweka wazi kuwa, yeye ni mdau mkubwa wa michezo, hivyo ameahidi kutoa ushirikiano kwa watumizhi wanamichezo, ili timu za halmashauri ziweze kufanya bizurinkatika mashindayo yote yatakayohusisha timu za halmashauri hiyo.
" Mimi ni mdau wa michezo, niwaahidi kutoa support kwa wachezaji na timu za halmsahuri pindi inapotokea kushiriki michezo yote"
Hata hivyo wachezaji hao, wamemshukuru mkurugezni huyo kwa kuwawezesha kushiriki mashindano hayo, mashindano ambayo timu hiyo iliibuka kidedea.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.