Na. Elinipa Lupembe.
Jumla ya watahiniwa 851 halmashauri ya Arusha, wanategemea kuanza mitihani yao ya taifa ya kidato cha sita na vyuo vya Ualimu leo 03.05. 2021, kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa na Baraza la Mitihani la Taifa -NECTA.
Akizungumza na mwandishi wetu, Mwenyekiti wa Kamati ya Mtihani, halmashauri ya Arusha ambaaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya Arusha, Saad Mtambule, amethibitisha jumla ya watahiniwa 851, watafanya mitihani yao taifa ya kuhitimu kidado cha sita na vyuo vya Ualimu katika halamshauri hiyo kwa mwaka wa masomo 2021, kwa kuzingatia ratiba iliyotolewa na Baraza la Mitihanainla Taifa -NECTA.
Mwenyekiti Mtambule, amesisitiza kuwa maandalizi yote yamekamilika kwa mujibu wa sheria na taratibu za mitihani ya Taifa na kuwataka wasimamizi wa mitihani hiyo, kufanya kazi hiyo maalumu kwa kuzingatia maelekezo yaliyotolewa kwenye semina elekezi, huku akiwasisitiza kujiepusha na vitendo vya udanganyifu katika mitihani hiyo kwani ni kinyume na sheria Za nchi.
"Kamati imepitia vituo vyote na kuzungumza na watahini, huku ikijiridhisha na maandalizi yote, niwasisitize wasimamizi wa mitihani kufuata maelekezo, taratibu zote za mitihani na kujiepusha na vitendo vya udanganyifu kwa kuwa haruhusiwi mtu yoyote kushiriki udanganyifu au kuwezesha udanganyifu katika mitihani".Amesisiatiza Mwenyekiti huyo wa Kamati ya Mtihani.
Naye Afisa Elimu Sekondari, halmashauri ya Arusha, mwalimu Menard Lupenza amefafanua kuwa, idadi hiyo ya watahiniwa 851, wapo watahiniwa wa shule 'school candidates' watahiniwa binafsi 'private candidates' pamoja na watahini wa vyuo vya ualimu ngazi ya Cheti na Stashahada.
Aidha ameweka wazi kuwa kati ya hao 851, watahiniwa 686 ni wa shule, wakiwa wavulana 323 na wsichana 383 na kufanya mitihani kwenye shule 11 za sekondari, watahiniwa 143 ni wa binafsi, wakiwa wavulana 56 na wasichana 87, wakifanya mitihani yao kwenye vituo 4 na watahiniwa 22 ni wa vyuo vya Ualimu, wavulana 12 na wasichana 10 wakifanya mitihani kwenye vituo 2.
Awali, uongozi wa halamshauri ya Arusha unawatakia kila la kheri watahiniwa wote, katika mitihani yao ya kuhitimu kidato cha sita na vyuo vya Ualimu kwa mwaka wa masomo 2021.
KILA LA KHERI WATAHINIWA WOTE WA KIDATO CAH SITA NA VYUO VYA UALIMU NGAZI YA CHETI NA STASHAHADA
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.