Na Elinipa Lupembe
Wajumbe wa Mabaraza ya Usuluhishi ya kata, wametakiwa kufanyakazi kwa kuzingatia taratibu zilizoainishwa kwenye miongozo iliyotolewa na serikali, ili kufanya mashauri kwa weledi na kwa kuzingatia haki.
Rai hiyo imetolewa na Mkurugenzi Mtendaji, halmashauri ya Arusha, Seleman Msumi, wakati wa mafunzo ya siku mbili ya wajumbe hao, yaliyofanyika kwenye ukumbi wa mikutano shule ya msingi Green Acres kwa kuwataka wajumbe hao, kutambua kuwa wanaufungua ukurasa mpya wa kwa kufanya usuluhishi wa migogoro ya ardhi kwenye maeneo yao.
Mkurugenzi Msumi amewataka wajumbe hao kutumia busara na hekima katika kufanya usuluhishi kwa kuzingatia Sheria, Kanuni na taratibu za Mabaraza ya usuluhishi, na pale inapotokea sintofahamu rudini kwenye miongozo inayowaelekeza nini cha kufanya.
"Mafunzo mliyopewa yazingatieni ili tukatende haki kulingana na taratibu zilizowekwa, majukumu mliyokasimiwa yanagusa maslahi ya jamii, familia na mtu mmoja mmoja kwa kutambua kanda hii ya Kaskazini hususan mkoa wa Arusha kuna migogoro mingi ya ardhi, kutokana na ufinyu wa ardhi usioendana na idadi ya watu, ni vymea kuzingatia taratibu za usuluhishi" AmesemaMsumiA
Aidha amewataka wajumbe hao, kutambua kuwa lengo la serikali ni kuhakikisha migogoro ya ardhi inatatuliwa kuanzia ngazi ya kijiji, kata na wilaya, hivyo jukumu kubwa wanalotakiwa kulitekeleza ni kwa manufaa ya wananchi na nchi kwa ujumla.Kwa sasa mambaraza yanafanya kazi ya usuluhishi na upatanishi na sio maamuzi, maamuzi yanatakiwa kuoelekwa kwenye ngazi nyingine za maamuzi kulingana na sheria na miongozo .
Hata hivyo wajumbe hao wameishukuru na kuipongeza serikali kwa mafunzo hayo na kuweka wazi kuwa miongozo na taratibu walizopewa zimewapata maarifa mapya, ambayo yatakuwa nguzo yao katika utendaji wa kazi zao za usuluhishi wa migogoro ya ardSes
Sesilia Msingwa mjumbe wa Baraza la Usuluhishi kata ya Oldonyosambu amesema kuwa mafunzo hayo yamewajengea uwezo wa kutambua namna ya kufanya usuluhishi kwa kuzingatia haki ya kila upande bila upendeleo na kuwafanya kujiamini na kutenda haki kwa watu wakati wa kufanya usuluhisMa.
"Mafunzo haya yametupa mwanga wa namna bora ya kusuluhisha migogoro kwa kuzingatia kanuni na taratibu, na zaidi yametuelekeza mipaka ya wajumbe kwamba kazi yao ni usuluhishi na si kufanya maamuzi" Thomas Kisioki Katibu Baraza la Usuluhishi kata ya Laroi
Hata hivyo Mkuu wa Kitengo cha Sheria, halmashauri ya Arusha Monica Mwailolo amesema kuwa, mafunzo hayo ni muhimu, yakiwa na lengo la kuwajengea uwezo wajumbe wa Mabaraza ya usuluhishi ya kata, Mabaraza ambayo yamepewa jukumu la usuluhishi wa migogoro ya Ardhi kulingana na Sheria ya Mabaraza ya Kata sura ya 206 na Sheria ya Mahakama za Ardhi sura ya 216.
Aidha amewataka wajumbe hao, kufanyakazi kwa karibu na kitengo cha sheria ili kuweza kutatua changamoto zozote zitakazojitokeza wakati wa mashauri.
"Niwatake wajumbe kuzigatia taratibu zilizowekwa kwa kuwa ndio nguzo zitakazowawezesha kufikia malengo ya kusuluhisha migogoro ya ardhi katika maeneo yenu" Amefafanua Mwanasheria Monicai
Awali uongozi wa halmashauri unawashukur wadau wote walioshiriki kuandaa mafunzo hayo, wakiwemo shirika la SOS Children, CWCD, PRINGO'S, Kituo cha Haki za Binadamu .
ARUSHA DC NI YETU, TUSHIRIKIANE KUIJENGA
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.