Na Elinipa Lupembe
Wanafunzi 1,544 shule ya msingi Matimu halmashauri ya Arusha wamepata msaada wa vifaa vya shule kutoka kwa Kampuni ya Utalii la Masaai Wounders la Jijini Arusha.
Akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi vifaa hivyo, Mkurugenzi Mkazi, Mwl. Ang'weni Lang'o, amebainisha kuwa, lengo la kugawa vifaa hivyo ni baada ya kuona changamoto inayowakabili baadhi ya wazazi ya kushindwa kumudu kuwapatia watoto wao vifaa vya shule.
Amesema kuwa kutokana na changamoto hiyo shirika likaona ni vema kuwapunguzia wazazi mzigo huo ili watoto waweze kupata nafasi ya kuhudhuria masomo yao bila kikwazo.
"Leo tumetoa sare za shule kwa wanafunzi wote 1,544 wa shule hii, jozi 1300 za viatu, mashati, sketi, suruali na masweta, nguo za michezo na vifaa vya michezo, pamoja na vitabu vya kiada kwa shule jirani ya sekondari Mukulat" . Amesema Mwl. Lang'o.
Naye mgeni rasmi Kaimu Mkurugenzi na Mkuu wa Idara ya Utawala na Rasilimali Watu, Elizabeth Ngobei licha ya kulishukuru shirika hilo amewataka wanafunzi kutumia fursa hiyo adhimu kusoma kwa bidii kwa kuwa, tayari wadau kwa kushirikiana na Serikali, wameshafanya sehemu kubwa ya majukumu yao.
Amewataka kutambua kuwa wapo watoto wenzao wanaoshindwa kuhudhuria shule kwa kukosa vifaa vya shule, na kuwasisitiza kuthamini fursa hiyo waliyopata kwa kuongeza bidii katika masomo yao ili kuzifikia ndoto zao.
"Wazazi mnalojukumu kubwa kuwasimamia watoto hawa kutunza vifaa hivi lakini walimu mnao wajibu wa kuhakikisha mnawafunfisha wanafunzi hawa ili waweze kufaulu vema na kufikia" Amesisitiza Elizabeth.
Hata hivyo wanafunzi hao wameshukuru shirika kwa misaada mingi inayotolewa shuleni hapo na kuahidi kusoma kwa bidii kwa kuwa shule yao ina mazingira mazuri na rafiki ya kujifunzia tofauti na shile nyingine za msingi.
Upendo Paulo mwanafunzi wa darasa la VI, amesema ndoto yake ni kuwa daktari hivyo ameahidi kusoma kwa bidii na kufikia ndoto yake kama ilivyo kwa watoto wengine wanaosoma shule za kulipia.
"Shule yetu ni nzuri sana, haina tofauti na shule za 'English Medium', mazingira ni mazuri, tuna vitabu, vifaa vya michezo na leo tumepewa uniform, kazi yetu ni kusoma kwa bidii". Ameweka wazi Enock Eliasi darasa la VI.
Hata hivyo Mwenyekiti wa Kamati ya shule Philemon Loth, hakusita kuwashukuru wadau hao kwa mambo makubwa wanayoyafanya shuleni hapo, na kuahidi kushirikiana na walimu kuhakikisha watoto wanahudhuria shule pamoja na kufanya vizuri katika masomo.
"Tunawashukuru wadau wetu, zaifi pia tunaishukuru Serikali yetu kwa kuweka mazingira rafiki kwa wadau na kufikiwa na msaada huu, sisi kama wazazi tunauthamini na tunaahidi kuwahimiza watoto wetu kuongeza bidii kwenye masomo kwa manufaa yao na Taifa". Amefafanua Mwenyekiti huyo.
Kampuni ya Masaai Woundering imekuwa ikitoa misaa mingi katika shule hiyo, ikiwemo uboreshaji wa miundombinu ya shule, chakula cha walimu na wanafunzi, vifaa na vitabu vya kufundishia na kujifunzia, pamoja na vifaa vya michezo.
ARUSHA DC Yetu, Tushirikiane Kuijenga'
KaziInaendelea ✍✍
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.