Katika hali isiyokuwa ya kawaida wananchi wa kijiji cha Olkokola wanaonyesha kukataa kata kata kupokea mradio wa maji wa vijiji vitano unaotegemewa kutekelezwa ndani ya kijiji chao kwa madai kuwa mradi huo umesanifiwa kutumia vyanzo vyao vya maji vya Tiasilele na Nadung'oro na kuwa wananchi hawana uwezo wa kulipia gharama za maji.
Jambo la kusikitisha zaidi hata wanawake wa Olkokola wanaotumia muda mwingi kuchota maji wamekuwa mstari wa mbele kukataa mradi huo wa maji licha ya Kauli Mbinu na mipango ya Wizara ya Maji na Umwagiliaji ya "MTUE MAMA NDOO" na lengo la kuhakikisha maji yanapatikana umbali usiozidi mita 400 na mwanamke.
Wananchi wa hao wamekataa kupokea mradi huo kwenye Mkutano wa kijiji licha ya kuwa Timu ya Watalamu wa halmashauri ya Arusha kuwaelezea namna mradi utakavyotekelezwa na juu ya Sera ya Serikali ya mwaka 2002 na sheria namba 12 ya mwaka 2009 ya kulipia huduna ya maji.
Aidha wananchi wanapaswa kufahamu kuwa Rasilimali maji ni mali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kulingana na Sheria namba 11 ya mwaka 2009 kifungu cha 10 hivyo mtu yoyote anaruhusiwa kutumia kwa mujibu wa sheria.
Mradi huo wa maji unatekelezwa kwenya vijiji viwili na vitongiji vitatu kupitia Shirika la WaterAid kwa ufadhili wa Idara ya Maendeleo ya Uingereza 'DFID' kwa mwaka wa fedha 2017/2018.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.