Wananchi na wakazi wa Kata ya Nduruma wameshiriki kwa hiari kwenye ujenzi wa Miundo mbinu ya Kituo cha Afya kama mchango wao katika ujenzi wa kituo chao cha Afya.
Akizungumza mbele ya wajumbe wa Kamati ya Fedha Utawala na Mipango walipotembelea kukagua utekelezaji wa Mradi huo Afisa Mtem=ndaji wa Kata ya Nduru ndugu Loisulye Mollel amesema kuwa waanchi wa nduruma wameshiriki kwenye ujenzi kwa kupoangiana zamu kwa kwa vijiji vyote ndani ya kata hiyo.
Loisulye amefafanua kuwa wananchi hao wanapangiana zamu kwa kutumia muda wa saa mbili mpaka tatu kufanya kazi kwa siku kila inapohitajika nguvu yao katika ujenzi huo na kuongeza kuwa wananchi hao wameridhishwa na kushirikishwa kwa kufanya kazi kama vibarua kwenye ujenzi huo ambao umeghari kiasi cha shilingi milioni 500 fedha zilizotolewa na serikali kwa jaili ya kuendeleza kituo hicho kwa lengo kuboresha huduma za afya na kuondoa vifo vya mama namtoto.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.