Elinipa Lupembe.
Wanaume katika jamii, wamehimizwa kusimama imara kutokomeza na kuachana na mila potofu zinazosababisha vitendo vya ukatili dhidi ya watoto, hususani watoto wa kike, dhamana ambayo iko mikononi mwa wanaume ambao ni viongozi wa familia na viongozi wa mila pia.
Hayo yamesemwa na Kaimu mkurugenzi, halmashauri ya Arusha, mwalimu Hossein Mghewa, wakati akifunga mafunzo ya siku tatu ya kupinga ukatili dhidi ya watoto, ukatili unaosababishwa na mila na desturi potofu za jamii, mafunzo yaliyoandaliwa na Wizara ya Afya, Jinsia, Wazee na watoto, Idara ya Ustawi wa Jamii, yaliyofanyika kwenye ukumbi wa mikutano halmashauri ya Arusha.
Kaimu mkurugenzi huyo, amesema kwamba, wanaume ndio viongozi na nguzo kuu za familia, na viongozi wa mila, hivyo wakiamua kubeba dhamana ya kufanya mabadiliko ya kijamii ya kuachana na mila potofu zinazosababisha ukatili dhidi ya watoto, vitendo hivyo vitapungua kwa kasi na hatimaye kutokomea kabisa.
Ameweka wazi kuwa, wanaume ndio watawala na wafanya maamuzi kuanzia ngazi ya familia na jamii, endapo wakiamua kwa pamoja kubadilika na kuachanan na mila hizo potofu za kukeketa na kuwaozesha watoto wa kike katika umri mdogo, ukatili utatoweka kabisa na kubaki historia kwenye jamii za kimaasai.
"Kama kila mwanaume ndani ya familia akisema, mtoto wangu wa kike, hatakeketwa wala kuolewa katika umri mdogo, hakuna anayeweza kupinga, na zaidi wale viongozi wa mila wakiamua ni marufuku mtoto wa kike kukeketwa, na wanaume wote wakatae kuoa msichana aliyekeketwa, mila hiyo itatokomea na wanawake watatii na jamii nzima itafuata na hatimaye ukatili huo utakwisha ndani ya jamii zetu". Ameweka wazi Kaimu huyo Mkurugenzi
Aidha ametoa wito kwa washiriki wote wa mafunzo hayo, kuwa mstari wa mbele kukemea vitendo vya ukatili katika maeneo yao, pamoja na kutumia maarifa waliyoyapata kushirikiana na serikali kuelimisha jamiii juu ya madhara ya ukatili dhidi ya watoto na kutoa taarifa katika mamalaka husika pindi mtoto atakapofanyiwa ukatili.
Hata hivyo washiriki wa mafunzo hayo licha ya kuipongeza serikali kwa kuandaa mafunzo hayo yaliyowapa maarifa kwa uwanda mpana, maarifa yaliyowawezesha kufahamu madhara ya ukatili kwa watoto na namna ya kupambana na ukatili, kwa kujikita kuelimisha jamii kila mtu kwa nafasi yake aliyonayo katika jamiii, lakini pia wamekiri kuwa wanaume wanayo dhamana kubwa ya kuweza kuleta mapinduzi ya kuachana na mila potofu za ukeketaji na ndoa za utotoni.
Mwenyekiti wa mafunzo hayo, Mchungaji Ezekiel Megiroo wa kanisa la KKT usharika wa Kisongo, Mchungaji Ezekiel Megiroo kutoka kkt Kisongo, amekiri kuwepo kwa vitendo vya ukatili vinavyofanywa na watu wa ndani ya familia na kuongeza kuwa, jamii inahitaji kupata elimu zaidi juu ya madhara makubwa ya ukatili huo, na kupitia mafunzo hayo na kutekeleza mpangokazi uliowekwa kwa weledi, utapunguza matukio ya ukatikli kwa asilimia kubwa
"Tuko tayari kutumia majukwaa yetu, kueleimisha jamii hususani wanaume ambao ndio viongozi wa familia, kubadili mitazamo yao na kuachana na mila potofu, jambo ambalo ninaamini litasaidia kuondokana na ukatili dhidi ya watoto kuanzia ngazi ya familia na jamii kwa ujumla wake"amesisitiza mchungaji Megiroo.
Naye mratibu wa mafunzo hayo, kutoka Wizarla ya Afya na Maendeleo ya Jamii, Imeldaevaeline Kamugisha, amesema kuwa, lengo la mafunzo hayo ni kujengeana uelewa wa pamoja wa kutokomeza ukatili dhidi ya watoto, na kuandaa mpango kazi kwa mwaka, ambao utafanyiwa fuatilaji wa utekelezaji wake mara kwa malrai ili kupata matokeo chanya na kufikia lengo la serikali la kuotokomeza ukatili unaokabili watoto katika jamii.
Mafunzo hayo ya siku tatu, yamejuisha watalamu wa Ustawi na Maendeleo ya Jamii na halmashauri ya Arusha, wajumbe wa kamati ya MTAKUWAA, polisi wa Dawati la Jinsia, Afisa Uhamiaji, walimu wa mangariba, wawakilishi wa makundi ya kijavmii, wadau wa mashirika yanaoyojihusisha na masuala ya ukatili, viongozi wa dini pamoja na viongozi wa mila.
ARUSHA DC
Kazi inaendelea✍✍
Kaimu mkurugenzi halmashauri ya Arusha, mwalimu Hossein Mghewa akifunga mafunzo ya siku tatu ya kupambana na ukatili dhidi ya watoto, mafunzo yaliyoandaliwa na Wizara ya afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, yaliyofanyika kwenye ukumbi wa mikutano, halmashauri ya Arusha.
Mwenyekiti wa washiriki wa mafunzo mchungaji Ezekiel Megiroo wa kanisa la KKT usharika wa Kisongo, akizungumza wakati wa kuahirisha mafunzo hayo ya siku tatu.
Mratibu wa mafunzo kutoka Wizara ya Afya -Idara ya Ustawi wa Jamii, Imeldaevaline Kamugisha akizungumza wakati wa kufunga mafunzo.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.