Na. Elinipa Lupembe.
Wazazi wametakiwa kutimiza majukumu yao katika kulea watoto wao na kuacha kufanyia ukatili kwa mikono yao wenyewe, kwa kuacha kuwalipia watoto wao chakula cha mchana, wawapo shuleni, kwa dhana potofu ya kuwa, serikali inawahudumia watoto kwa kutoa elimu bure.
Rai hiyo imetolewa na mkurugenzi Mtendaji, Halmashauri ya Arusha, Dkt, Wilson Mahera, wakati akifungua warsha ya siku tatu ya Kamati ya Ulinzi na Usalama wa Mtoto MTAKUWWA halmashauri ya Arusha, amesema kuwa, wazazi wamekuwa na tabia ya kuwafanyia ukatili watoto wao, kwa kuwanyima, chakuka cha mchana wawapo shuleni, kwa madai ya kuwa elimu ni bure, jambo ambalo ni kinyume na taratibu.
Ameongeza kuwa,serikali na mashirika yasiyo ya kiserikali, wamekuwa mstari wa mbele kutetea haki za watoto na kupambana na ukatiti dhidi ya watoto lakini bado baadhi ya wazazi wamekuwa kikwazo kwenye harakati hizo, kwa kushindwa kwa makusudi kuwalipia chakula cha mchana wawapo shuleni, kwa madai kuwa elimu ni bure, jambo ambalo linakwamisha juhudi za serikali pamoja na kudhorotesha kiwango cha ufaulu kwa watoto.
"Kwa tabia ya kutokumpa mtoto chakula cha mchana huo ni ukatili, haiwezekani mtoto kushinda na njaa, kuanzia asubuhi mpaka jioni akiwa shuleni, halafu useme unampenda mtoto wako, huo ni ukatili na unapaswa kuachwa mara moja" amesema mkurugenzi.
Aidha amewasihi wazazi kuwaonea huruma watoto wao, na kutambua kuwa Sera ya elimu bila malipo, inaweka wazi majukumu ya serikali na majukumu ya mzazi kwa mtoto, ikiainisha jukumu la mzazi ni pamoja na kumpatia mtoto chakula cha mchana kwa shule za kutwa, kumpatia vifaa vya shule na mahitaji yake yote ya msingi.
Naye Mkurugenzi wa Shirika la Kijiji cha Watoto SOS, Grace Nkya, amesema kuwa shirika lake linajihusisha na kupambana na ukatili dhidi ya watoto kwa kuwalea na kuwahudumia, watoto wanaoshi kwenye mazingira hatarishi na kuwaundia familia ili aweze kuishi kama yuko nyumbani.
Nao wajumbe wa Kamati hiy ya MTAKUWA wamethibitisha kuwa moja ya changamoto inayowakabili wazazi ni kuweka viapumbele kwenye masuala yasiyo ya muhimu ambayo hugharimu pesa nyingi na kushindwa kukidhi mahitaji ya watoto.
Wamefafanua kuwa, wazazi wako radhi kuchangia fedha nyingi kwenye harusi na mbesii 'kumsalimia mtoto aliyezaliwa', na kushindwa kuchangi chakula cha mchana cha mtoto wake, jambo ambalo wamethibitisha ni ukatili unaofanywa wazi kabisa na wazazi.
"Ni rahisi kabisa, kutoa shilingi laki moja mpaka tano, kuchangia harusi au mbesii moja, na kutelekeza kulipia chakula cha mtoto cha shilingi laki moja kwa mwaka mzima" wamesema wajumbe hao.
Aidha wameitaka jamii sasa, kubadilika na kuanza kuwekeza fedha nyingi kwenye elimu na sio kwenye masuala ya kijamii, ambayo kimsingi ni ya muda mfupi na hayana tija kwa taifa letu la Tanzania.
Hata hivyo, Afisa Ufisa Ustawi wa Jamii, mkoa wa Arusha, Denis Mgiye, amesema kuwa, lengo la mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo wajumbe wa kamati ya MTAKUWWA wilaya, kupambana na ukatili dhidi ya watoto pamoja na kubadilishana changamoto zinazowakabili watoto.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.