Na Elinipa Lupembe
Wazee halmashauri ya Arusha wakipima afya zao kwa magonjwa yasiyoambukiza wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Wazee Duniani 2023 kiwilaya yaliyofanyika kijiji cha Nduruma kata ya Nduruma
Katika maadhimisho hayo wazee walipata huduma za kupima afya bure kwa magonjwa yasiyoambukiza ikiwemo pressure, kisukari na uzito, huku wakihamasihwa kupima magonjwa hayo mara kwa mara.
Mganga Mkuu wa halmashauri ya Arusha Dkt. Petro Mboya amesema kuwa ni muhimu wazee kupima afya zao mara kwa mara kiwemo magonjwa yasiyoambukiza ambayo yanawashambulia wazee kutokana na kinga za mwili kupungua, kwa kufanya hivyo kutawawezesha kuishi kulingana na hali za afya zao,
Hata hivyo Dkt. Mboya amewasisitiza wazee hao kuzingatia matumizi ya lishe bora kwa wazee kwa kula mlo kamili zaidi mbogamboga na matunda na kupunguza vyakula vya wanga, huku wakizingatia kuushughulisha mwili kwa kufanya kazi na mazoezi madogomadogo kama kutembea na sio kukaa na kulala
Awali Maadhimisho ya Siku ya Wazee yana lenga kuhamasisha jamii kuongeza uelewa wa juu ya masuala yanayohusu uzee na kuzeeka ikiwemo haki zao na upatikanaji wa huduma muhimu kwa wakati.
Kauli mbiu:"Udhibiti wa Wazee kwenye Dunia yenye mabadiliko"
ARUSHA DC NI YETU, TUSHIRIKIANE KUIJENGA
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.