Mazingira bora ni nyenzo muhimu katika tendo la kujifunzia kwa mwanafunzi na kufundishia kwa mwalimu na ambayo huleta hamasa kwa mwanafunzi kujifunza kupitia milango yote ya fahamu. Serikali ya awamu ya sita imetekeleza kwa vitendo uwepo wa mazingira bora ya kujifunzia na kufundishia kwenye shule za sekondari nchini, kwa kujenga vyumba 8,000 vya madarasa maalum kwa ajli ya wanafunzi kwa kidato cha kwanza 2023.Halmashauri ya Arusha ni miongoni mwa halmashauri nchini, iliyopokea kiasi cha shilingi milioni 760 kwa ajili ya ujenzi wa vyumba 38 vya madarasa kwenye shule 18 za sekondari za halmasahuri hiyo.Mkurugenzi Mtendaji halmashauri ya Arusha, Seleman Msumi, amekiri kupokea kiasi hicho cha fedha kilichotumika kujenga vyumba 38 vya madarasa, viti na meza za wanafunzi, pamoja na ofisi 7 za walimu kwenye shule 6 kati ya shule hizo 18.Hata hivyo viongozi wa chama na serikali wa halmashauri ya Arusha wamezungumzia ufahari wa mradi huo wa ujenzi wa vyumba vya madarasa kwa ajili ya wanafunzi wa kidato cha kwanza mwaka 2023.Mkuu wa wilaya ya Arumeru Mhandisi Richard Ruyango amesema kuwa, uwepo wa vyumba vya madarasa umewapa fursa na kuwahakikishia wanafunzi 7,856 waliofaulu mtihani wa darasa la saba mwaka 2022 na kupangiwa shule za sekondari za serikali halmashauri ya Arusha sawa na 100% kuanza shule kwa wakati mapema Januari 9 kwa mujibu wa ratiba ya masomo ya mwaka huo.Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi wilaya ya Arumeru, Komredi Noel Severe amewapongezwa watalamu, viongozi pamoja na wananchi kwa kusimamia vema Ilani ya CCM, utekelezaji unaofanyika kupitia miradi ya maendeleo inayoletwa na serikali katika maeneo yao.Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Arumeru Magharibi, Mhe. Noah Lembris amesema kuwa katika kipindi cha awamu ya sita, Jimbo lake limepata fedha nyingi za kutekeleza miradi ya maendeleo tofauti na awamu zilizotangulia.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.