Serikali kupitia Ofisi ya Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania imetoa madawati 400 kwa halmashauri ya Arusha kwa ajili ya kukabiliana na changamoto ya upungufu wa madawati katika shule za serikali.
Mwenyekiti wa halmashauri ya Arusha mheshimiwa Noah Lembris ameishukuru serikali kwa msaada huo kwa kuwa halmashauri bado inakabiliwa na upungufu wa madawati kutokana na ongezeko kubwa la wanafunzi walioandikishwa kwa miaka miwili mfululizo sasa.
Afisa Elimu Msingi halmashauri ya Arusha mwalimu Tumsifu Mushi amesema madawati hayo yamekuja wakati muafaka kwa kuwa katika shule za msingi kuna upungufu wa madawati 840 na kueleza kuwa upungufu huo umetokana na uandikishwa wa wanafunzi 13,030 sawa na asilimia 135.8% kwa mwaka huu 2017 idadi hyo ni ongezeko la asilimia 25% ya wanafunzi walioandikishwa mwaka jana wa 2016 na Madawati hayo yatakugawanywa kwenye shule zenye upungufu zaidi kwa kulinganisha na nyingine.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.