Wakurugenzi wa Halmashauri ya Arusha na Meru, wanawatangazia wananchi wote, ikiwemo watu binafsi, Taasisi, Mashirika, Makampuni na Vikundi, wenye nia ya kupanga nyumba, kwenye jengo lao katika kiwanja namba 17 eneo la Engira karibu na Kibo Palace Hotel ( Uzunguni) katika Jiji la Arusha.
Mwombaji atatakiwa kuchukua Kabrasha la Zabuni katika Ofisi ya Bodi ya Zabuni za halmashauri ya Arusha, Zabuni zitatolewa kuanzia tarehe 24/02/2020, Jumatatu mpaka Ijumaa, muda wa saa za kazi kuanzia 01:30 asubuhi mpaka saa 09:30 alasiri.
Mwisho wa kupokea maombi hayo ni tarehe 16/03/2020 saa 04:00 asubuhi.
Waombaji wanaalikwa kuhudhuria ufunguzi wa Zabuni hizo, utakaofanyika muda mfupi baada ya saa 04:00 tarehe ya mwisho wa kupokea maombi, Ufunguzi utafanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano halmashauri ya Arusha.
******Jengo hili linamilikiwa na halmashauri ya Arusha na Meru********
Soma barua kwa maelezo zaidi.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.