Friday 9th, May 2025
@Arusha DC
Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Mheshimiwa Jerry Muro, anawatangazia wananchi wote kushiki mbio za Mwenge wa Uhuru 2019, utakaowasili kesho tarehe 08.06.2019, kwenye Halmashauri ya Arusha, wilaya ya Arumeru.
Katika Halmashauri ya Arusha, Mwenge wa Uhuru 2019, utapokelewa saa 02:00 asubuhi, kwenye viwanja vya shule ya msingi Oldonyowas kata ya oldonyowas, ukitoke wilaya ya Longido.
Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa 2019, Ndugu Mzee Mkongea Ali, atakimbiza Mwenge wa Uhuru umbali wa Kilomita 64.4 na kukagua jumla ya miradi 8, yenye thamani ya shilingi bilioni 15.9, miradi iliyolenga sekta ya Maji, Elimu, Afya, Mazingira, Mifugo na Viwanda.
Wananchi wote mnaombwa kushiriki mbio za Mwenge wa Uhuru 2019 kwenye maeneo ya Miradi ya maebdeleo na baadaye kwenye sherehe za mkesha zitakazofanyika kwenye viwanja vya ofisi za Makao Makuu ya Halmashauri ya Arusha eneo la Sekei, na kesho yake kukabidhi halmashauri ya Meru.
Kauli Mbiu ya Mwenge wa Uhuru 029" Maji ni Haki ya Kila mtu, tutunze vyanzo vyake na Tukumbuke kushiriki uchaguzi wa Serikali za Mitaa"
*Miradi itayokaguliwa ni kama inavyoonekana kwenye picha
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.