Friday 9th, May 2025
@Ukumbi wa Mikutano Arusha DC
Na. Elinipa Lupembe.
Mkurugenzi Mtendaji halmashauri ya wilaya ya Arusha,Dkt. Wilson Mahera, anawatangazia wananchi wote, kuhudhuria kwenye Mkutano wa Baraza la Madiwani (Full Council), utakaofanyika leo, tarehe 22.05.2019, kwenye Ukumbi wa Mikutano halmashauri ya Arusha.
Mkutano huu ni wa kawaida kwa mujibu wa sheria za Serikali za Mitaa, utakaojadili shughuli za utekelezaji wa maendeleo kwa kipindi cha robo ya tatu kwa mwaka wa fedha 2018/2019, kipindi cha kuanzia mwezi Januari mpaka Machi, 2019.
Mkutano utakuwa na agenda 13, agenga kuu ikiwa ni pamoja na Maswali ya papo kwa papo, Kujadili taarifa za Mapato na Matumizi, taarifa za utekelezaji wa miradi ya maendeleo, kupokea na kupitisha mihitasari ya Kamati nne za kudumu za halmashauri, utekelezaji wa shughuli za maendeleo ya Mamlaka ya mji mdogo Ngaramtoni, pamoja na taarifa ya Rasimu ya motisha kwa watumishi.
Aidha, Mkurugenzi Mtendaji anawataka wananchi zote kuhudhuria mkutano huo unaojadili Maendeleo ya Halmashauri yao.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.