Friday 9th, May 2025
@UKUMBI WA MIKUTANO HALMASHAURI YA ARUSHA
Mkurugenzi Mtendaji, Halmashauri ya Arusha, Seleman Msumi, anawatangazia wananchi wote kuhudhuria Mkutano wa kawaida wa Baraza la Madiwani (Full Council), utakaofanyika tarehe 28.10.2021, kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri hiyo, kuanzia saa 03:30 asubuhi.
Mkutano huo ni wa kawaida kwa mujibu wa Sheria, Kanuni na Taratibu za Serikali za Mitaa, wenye lengo la kujadili utekelezaji wa shughuli za Maendeleo zilizotekelezwa katika Halmashauri kwa kipindi cha miezi mitatu na robo ya kwanza kwa mwaka wa fedha 2021/2022, kwa kipindi cha kuanzia mwezi Julai mpaka Septemba 2021.
Aidha Mkutano huo wa baraza la Madiwani utakuwa na ajenda 10, huku agenda kuu zikiwa ni pamoja na Maswali ya papo kwa papo,Taarifa za utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo kipindi cha robo ya kwanza mwaka wa fedha 2021/2022, bango kitita la sheria ndogo mpya za halmashauri, pamoja na Kupitisha Mihtasari ya Vikao vya robo vya Kamati za Kudumu za Halmashauri ya Wilaya ya Arusha.
Mkutano wa wazi, wananchi wote mnaalikwa kuhudhuria pamoja na kuendelea kuchua tahadhari za UVIKO 19.
NYOTE MNAKARIBISHWA!!
#KaziInaendelea
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.