Friday 9th, May 2025
@Ukumbi wa Mikutano Halmashauri ya Arusha
Mkurugenzi Mtendaji halmashauri ya wilaya ya Arusha, anawatangazia wote, kuhudhuria kwenye Mkutano wa Baraza la Madiwani (Full Council) , utakaofanyika siku ya Ijumaa tarehe 31.07.2018, kwenye Ukumbi wa Mikutano halmashauri ya Arusha.
Mkutano huu ni wa kawaida kwa mujibu wa sheria utakaojadili shughuli za utekelezaji wa maendeleo kwa kipindi cha robo ya nne cha kuanzia mwezi Aprili mpaka Juni, 2018.
Agenda kuu katika Mkutano huo ni pamoja na Maswali ya papo kwa papo, Kujadili taarifa za Mapato na Matumizi, taarifa za utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwa kipindi cha miezi mitatu ya robo ya nne, kupokea na kupitisha mihitasari ya Kamati nne za kudumu za halmashauri pamoja na utekelezaji wa shughuli za miradi ya maendeleo ya Mamlaka ya mji mdogo Ngaramtoni.
Aidha, Mkurugenzi Mtendaji anawataka wananchi zote kuhudhuria mkutano huo unaojadili Maendeleo ya Halmashauri yao.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.