Friday 9th, May 2025
@Kata ya Oljoro
Mkuu wa mkoa wa Arusha, Mheshimiwa Mrisho Mashaka Gambo, anatarajia kufanya ziara ya kikazi kwa siku moja katika halmashauri ya Arusha wilayani Arumeru, siku ya Jumanne tarehe 04.09.2018.
Ziara hiyo ni ya kawaida katika kutekeleza majukumu ya kawaida ya kikazi ikiwa ni pamoja na kuzungumza na kuwasikiliza watumishi na wananchi wake, kukagua utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo kisekta huku ziara hii ikiwa maalumu kwa ajili ya kutembelea na kukagua Miradi katika sekta ya Afya.
Akiwa katika halmashauri ya Arusha mheshimiwa mkuu wa mkoa huyo, atapata fursa ya kuzungumza na watumishi halmashauri ya Arusha, atakagua Mradi wa ujenzi na upanuzi wa Kituo cha Afya Mbuyuni kata ya Oljoro na baadaye kuzungumza na wananchi kwenye mkutano wa hadhara, utakaofanyika katika Kijiji cha Mbuyuni kata ya Oljoro.
Wananchi wote wa kata ya Oljoro na kata za jirani mnaombwa kufika, kumsikiliza na kuzungumza na mkuu wenu wa mkoa.
"UONGOZI UNAOACHA ALAMA"
Raiba hii ni imetolewa na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.