Na Elinipa Lupembe
Afisa Programu shirika la Mtandao wa Wakulima na Wafugaji, mkoa wa Arusha (MVIWAARUSHA) Damiani Sulumo akiwa kwenye zaoezi la upandaji miti shule ya msingi Bwawani kata ya Bwawani, wakati wa kampeni ya upandaji miti 2023.
Ifahamike kuwa, halmashauri ya Arusha kwa kushikiana MVIWAARUSHA, wameendesha kampeni ya upandaji miti mwaka 2023 huku takribani miti laki moja ikitegemewa kupandwa kwenye vijiji 8 kwa awamu ya kwanza na kuendelea kwa vijiji vingine vya halmashauri hiyo.
Bwana Damiani, ameweka wazi lengo la MVIWAARUSHA ni kurejesha uoto wa asili ulioharibiwa kwa kukata miti, pamoja na kuzuia mmomonyoko wa udongo kwa kutengeneza mafanya juu na mafanya chini kwenye vilima na kupanda miti pamoja na makinga maji.
"Tumeshuhudia hali ya Ukame, huku tafiti zikionyesha baadhi ya maeneo ya halmashauri ya Arusha hali ya mazingira ikiendelea kuwa mbaya, tutumie fursa hii kuelekeza nguvu kurejesha uoto wa asili kwa kuotesha miti mingi kwenye mazingira yanayotuzunguka" Amesidiyiza Damiani
"Mti wangu, Taifa langu, Mazingira yangu, KaziIendelee"
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.