• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe |
Arusha District Council
Arusha District Council

Serikali ya jamuhuri ya Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili Makuu
    • Mikkati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara na Vitengo
      • Utawala na Utumishi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Fadha na Biashara
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliji
      • Ardhi na Maliasili
      • Maji
      • Works
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo na Umwagiliaji na Ushirika
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Internal Audit
      • Nyuki
      • Uchaguzi
      • UKIMWI/ AIDS
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Livestock
    • Wadau wa Maendeleo
  • Huduma Zetu
    • Health
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Utawala Fedha na Mipango
      • Elimu Afya na Maji
      • Kudhibiti UKIMWI
      • Maadili ya Madiwani
      • Uchumi Ujenzi na Mazingira
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Vikao vya Timu ya Uendeshji ya Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mktaba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa UMMA
    • Video za Shoghuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

Ahadi za ujenzi wa choo kipya,shule ya Msingi Seliani zaanza kutekelezwa

Posted on: November 2nd, 2018

Kufuatia tukio la kutitia kwa choo cha wanafunzi, shule ya Msingi Seliani, halmashauri ya Arusha wilayani Arumepru, Kampuni ya Eco Valley Advisers inayojihusisha na kampeni ya Nyumba ni Choo,  imetimiza ahadi yake kwa kutoa, msaada wa masinki 21 ya vyoo, yenye thamani ya shilling 253,000, kwa lengo kuchangia ujenzi wa choo kipya, mara baada ya kutitia kwa choo hicho.

Akikabidhi masinki hayo, kwa mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya Arusha, Meneja wa kampuni hiyo Avit Buchwa, amesema kuwa, wametoa masinki hayo baada ya kupata taarifa za kutitia kwa choo cha wanafunzi, kutoka kwa mkuu wa wilaya hiyo, Mheshimiwa Jerry Muro, wakaona ni vema kutoa msaada huo ili wanafunzi hao wapate mahali salama pa kujisaidia kwa haraka bila kuathiri ratiba yao ya masomo.

Meneja Buchwa, ametoa ufafanuzi juu ya masinki hayo kuwa, sinki 1 kati ya masinki 21 waliyoyatoa ni maalumu  kwaajili ya wanafunzi walemavu, huku masinki 20 yakiwa kwa ajili ya kuwahudumia wanafunzi wasio walemavu na kuongeza kuwa, masinki hayo yametengenezwa kwa malighafi ya plastiki ambayo ni rahisi kwa matumizi kwa watoto wa rika zote hivyo yataongeza usalama wa watoto pindi watakapokuwa wakitumia.

"Haya masinki yana kifuniko maalumu kinachotenganisha shimo na sehemu ya juu, hivyo ni salama kutumiwa hata na mtoto mdogo bila kuhofia kutumbukia, pia mfuniko huo unazuia harufu mbaya ya choo kutoka nje na pia kuzuia wadudu kama inzi na mende kuingia au kutoka chooni, hivyo ni salama zaidi kwa afya" amethibitisha Buchwa.

Pia ameongeza kampuni ya Eco Valley Advisers imeamua kutoa masinki hayo, ili kuunga mkono juhudi za serikali katika kuboresha miundombinu ya Elimu na kuwafanya watoto wa kitanzania kusoma katika mazingira salama na rafiki.

Hata hivyo ameishauri jamii kutumia masinki hayo kwaajili ya usalama wa afya zao, na kuwa gharama zake ni za chini kwa  mwananchi wa hali ya chini kumudu kununua, ukilinganisha na gharama kubwa za masinki za malumalu na pia matumizi yake ni rahisi hata kwebye maeneo yenye shida ya maji kwani hutumia maji kidogo.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya Arusha,  Dkt. Wilson Mahera, ameishukuru kampuni hiyo kwa kuwapatia masinki hayo, ambayo yatawezesha ukamilishaji wa ujenzi wa choo hicho mapema na wanafunzi kuanza kukitumia huku akiwataka wadau wengine wa maendeleo kujitokeza kuunga mkono juhudi za Serikali katika sekta ya Elimu.

Aidha amewaahidi kukuanza kutumia aina ya masinki, katika ujenzi wa vyoo vya shule hasa kwenye maeneo yanye shida ya maji na kwa kuwa ni rahisi kutumika kwa rika zote na zaidi yatasaidia kuwa na uhakika wa usalama wa mtoto pindi anapoyatumia.

Afisa mtendaji wa kata ya Kimnyaki, Joshua Jonas licha ya  kuishukuru kampuni hiyo kwa msaada huo, amethibitisha kuwa, tayari ujenzi wa choo hicho umeshaanza, na uko katika hatua za awali ya msingi, msingi ambao umechimbwa na wananchi wenyewe wa Kimnyaki.

Msaada huo wa masinki ya vyoo ni miongoni mwa ahadi za michango ya wadau mbalimbali, kufuatia tukio la kutitia kwa choo cha wanafunzi wa shule ya msingi Seliani, tukio lililotokea mwishoni mwa mwezi Oktoba mwaka huu.

Matangazo

  • TANGAZO LA KAZI ZA MKATABA HALMASHAURI YA WILAYA YA ARUSHA August 14, 2025
  • ORODHA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO 2023 ARUSHA DC June 11, 2023
  • ZIARA YA WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS TAMISEMI, MHE. MOHAMED O. MCHENGERWA 17 SEPTEMBA 2024 September 13, 2024
  • MTIHANI WA DARASA LA SABA 11-12/09/2024 September 09, 2024
  • Tazama zote

Habari mpya

  • KUFUATILIA NA USAMIZI WA HAKI ZA MTOTO KATIKA JAMII NI JAMBO MUHIMU

    August 25, 2025
  • RAIS SAMIA AMUAPISHA AMOS MAKALLA KUWA MKUU WA MKOA WA ARUSHA

    August 26, 2025
  • DKT. JAHANNES LEMBULUNG' LUKUMAY ACHUKUWA FOMU YA UGOMBEA UBUNGE WA CCM JIMBO LA ARUMERU MAGHARIBI

    August 25, 2025
  • KIKAO KAZI CHA WENYEVYITI WA BODI NA WATENDAJI WAKUU WA TAASISI ZA UMMA (CEOs Forum 2025)

    August 24, 2025
  • Tazama zote

Video

Video zaidi

Viunganishi vinavyoingiliana

  • Leseni ya vileo
  • Fomu ya ukaguzi

Viunganishi vinavyohusiana

  • Tovuti kuu ya serikali
  • Tamisemi
  • Utumishi portal
  • Wakala wa serikali mtandao
  • Mkoa wa arusha
  • ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Sekei Road

    Anuani ya posta: 2330 Arusha

    Simu : +255 027 2502737

    Simu: 073 65000476

    Barua pepe: ded@arushadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.