# Ameahidi kuanza na kushughulikia migogoro ya ardhi inayowakabili wananchi na kuwataka Madiwani hao, kuungana na Serikali ya awamu ya tano, kutatua migogoro ya ardhi huki akiwaonya kutokujihusisha na migogoro hiyo kwa maslahi yao binafasi kulingana na nafasi zao katika jamii.
# Amewataka Madiwani kubuni vyanzo vipya vya mapato pamoja na kushiriki kusimamimia ukusanyaji wa mapato katika maeneo yao, ili kuongeza kiwango cha ukusanyaji katika halmashauri hiyo.
# Amethibitisha kuwa ikiwa kutakuwa na usimamizi imara wa ukusanyaji wa mapato, kupitia vyanzo vya mapato vilivyo na kubuni vyanzo vingine vipya, halmashauri ya Arusha, inaweza kukusanya mapato zaidi na kuweza kufiisha kiasi cha shilingi billion kumi kwa mwaka.
#Endapo madiwani hawatashiriki katika usimamizi thabiti waukusanyaji wa mapato, ni dhahiri halmashauri italazimika kutolipa posho za madiwani hao pamoja na kuvunjwa kwa baraza la madiwani kutokana na wao kushindwa kutekeleza majukumu yao.
# Amewataka Madiwani kufanya kazi ya kuwatumikia wananchi, kwa weledi kwa kuzingatia kanuni, sheria na taratibu huku wakiendelea kutekeleza Ilani ya Chama tawala Chama kilichopo madarakani, Chama cha Mapinduzi.
# Ameagiza Idara ya Maendeleo ya Jamii kumpatia, taarifa ya mwenendo wa utoaji mikopo ya wanawake na vijana, mikopo ya asilimia kumi ya mapato ya ndani kwa kipindi cha miaka mitano ya nyuma kuanzia sasa, ili kuona vikundi ambavyo vilipatiwa mikopo hiyo huku akisisitiza utoaji wa mikopo hiyo kila baada ya makusanyo.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.