• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe |
Arusha District Council
Arusha District Council

Serikali ya jamuhuri ya Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili Makuu
    • Mikkati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara na Vitengo
      • Utawala na Utumishi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Fadha na Biashara
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliji
      • Ardhi na Maliasili
      • Maji
      • Works
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo na Umwagiliaji na Ushirika
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Internal Audit
      • Nyuki
      • Uchaguzi
      • UKIMWI/ AIDS
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Livestock
    • Wadau wa Maendeleo
  • Huduma Zetu
    • Health
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Utawala Fedha na Mipango
      • Elimu Afya na Maji
      • Kudhibiti UKIMWI
      • Maadili ya Madiwani
      • Uchumi Ujenzi na Mazingira
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Vikao vya Timu ya Uendeshji ya Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mktaba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa UMMA
    • Video za Shoghuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

DED Arusha DC aunga mkono juhudi za wananchi wake, katika ujenzi wa miundombinu ya shule.

Posted on: August 24th, 2019

Na. Elinipa Lupembe.

Katika kutekeleza mkakati wa Serikali ya awamu ya tano, wa kuboresha miundombinu ya shule na elimu kwa ujumla, halmashauri ya Arusha imeendelea kushirikiana na wananchi na wadau wa ndani na nje ya nchi, kuboresha miundombinu ya shule kwa kuongeza kasi katika ujenzi wa vyumba vya madarasa pamoja ujenzi wa shule mpya za sekondari.

Akijibu swali lililoulizwa na diwani wa kata ya kimnyaki, mheshimiwa  Olais Wavii, wakati wa mkutano wa Baraza la Madiwani wa robo ya nne, aliyetaka kufahamu ni namna gani halmashauri imejikita katika kutatua changamoto ya upungufu wa vyumba vya madarasa, ilihali wananchi wamekuwa mstari wa mbele kutoa michango kwa hiari na kujenga vyumba vya madarasa, katika maeneo yao.

Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri hiyo, Dr Wilson Mahera, mesema serikali inatambua juhudi zinazofawanywa na wananchi katika kuhakikisha wananafunzi wanapata elimu kwenye mazingira rafiki, hivyo halmashauri inashirikiana na Wadau mbalimbali wa maendeleo na kupata vifaa vya ujenzi, vitakavyowezesha kukamilisha ujenzi wa maboma hayo.

Aidha amefafanua kuwa kwa robo hiyo ya nne, wamepata jumla ya mifuko 180 ya saruji, ikiwa mifuko  100 imetolewa na Mbunge Viti maalum, mheshimiwa  Amina mollel, mifuko 60 imetolewa na Mkuu wa wilaya ya Arumeru, mheshimiwa Jerry Muro, na mifuko 20 imetolewa na benki ya CRDB tawi la Sekei, na bado wanaendelea kutafuta wadau wengine kwa ajili ya ukamilishaji wa miundombinu hiyo.

Hata hivyo Dkt. Mahera amezitaja baadhi ya shule za sekondari ambazo zimeonekana kuwa na upungufu wa vyumba vya madarasa,   ikiwemo sokoni II, Kiranyi, Nduruma na Lengijave, na kueleza kuwa, tayari ujenzi wa vyumba vya madarasa umefanyika na kufikia baadhi yake kufikia hayua ya boma, na mkakati uliyopo ni kukamilisha maboma hayo, ili ifikapo Januari 2020, wanafunzi wa kidato cha kwanza waanze shule bila kikwazo.

"Tutahakikisha hadi kufikia mwakani 2020 ujenzi wa vyumba vya madarasa vinakamilika kwa wakati, tayari kwa kupokea wanafunzi wa kidato cha kwanza, darasa la kwanza na madarasa ya Awali ."alisema mahera

Mkurugenzi huyo hakusita kuwapongeza wananchi wa halmashauri hiyo, kwa kuona umuhimu wa kuwa na shule za sekondari katika maeneo yao, kwa kuwapunguzia watoto wao adha ya kutembea umbali mrefu na kuamua kujenga shule katika maeneo yao.

Na kuthibitisha kuwa, jumla ya shule tatu mpya za sekondari zinatarajiwa kuanza mwaka ujao wa masomo, ambapo wananchi wa kijiji cha Likamba kata ya Musa, wanajenga shule ya sekondari Likamba, wanachi wa kata ya Oldonyowas, wanajenga shule ya Losinoni Juu na wananchi wa kijiji cha Kiserian wamejenga shule ya sekondari ya Kiserian kwa makubaliano na chuo kikuu cha Mzumbe, mchakato wa usajili wa  shule hizo unaendelea kwa ajili ya kupokea wanafunzi mwezi Januari, 2020.

Ameongeza kuwa, ujenzi huo wa vyumba vya madarasa kwa baadhi ya shule za sekondari mpya na zile za zamani, unakwenda sambamba na umaliaziaji wa  ujenzi wa maabara za masomo ya Sayansi pamoja na ujenzi wa mabweni na maktaba  kwa baadhi ya shule.

Hata hivyo katika mkutano huo wa  Baraza la madiwani, umefanyika uchaguzi wa makamu mwenyekiti wa halmashauri hiyo ambapo, diwani wa kata ya Olturoto mheshimiwa Baraka Simon wa Chama Cha Mapinduzi, amechaguliwa kuwa Makamu Mwenyekiti na kuchukua nafasi ya diwani wa kata ya Oloirien mheshimiwa Albert Oltulele kwa tiketi ya CHADEMA. aliyeshika nafasi hiyo kwa kipindi cha mwaka mmoja.

Vyumba vya madarasa shule mpy ya Sekondari Likamba kata ya Musa, mradi unaotekelezwa kwa nguvu za wananchi wa kijiji cha Likamba na vitongoji vyake.

Nyumba ya walimu, shule mpya ya sekondari Likamba kata ya Musa,mradi unaotekelezwa kwa nguvu za wananchi wa kijiji cha Likamba na vitongoji vyake.

Vyumba vya madarasa shule ya sekondari Sikon II vinajengwa kwa ufadhili wa ubalozi wa Japan nchini Tanzania


Vyumba vya madarasa shule ya sekondari Kiranyi, mradi uliotekelezwa kwa nguvu za wananchi.

Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA MKATABA ENABOISHU FM - ARUSHA DC May 26, 2025
  • ORODHA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO 2023 ARUSHA DC June 11, 2023
  • ZIARA YA WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS TAMISEMI, MHE. MOHAMED O. MCHENGERWA 17 SEPTEMBA 2024 September 13, 2024
  • MTIHANI WA DARASA LA SABA 11-12/09/2024 September 09, 2024
  • Tazama zote

Habari mpya

  • DKT. PASCAL KATIKA WIKI YA UTUMISHI WA UMMA

    June 19, 2025
  • WIKI YA UTUMISHI WA UMMA

    June 18, 2025
  • MAADHIMISHO YA WIKI YA UTUMISHI

    June 17, 2025
  • VIONGOZI WA DINI WAPEWA ELIMU YA CHAKULA BORA

    May 28, 2025
  • Tazama zote

Video

Video zaidi

Viunganishi vinavyoingiliana

  • Leseni ya vileo
  • Fomu ya ukaguzi

Viunganishi vinavyohusiana

  • Tovuti kuu ya serikali
  • Tamisemi
  • Utumishi portal
  • Wakala wa serikali mtandao
  • Mkoa wa arusha
  • ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Sekei Road

    Anuani ya posta: 2330 Arusha

    Simu : +255 027 2502737

    Simu: 073 65000476

    Barua pepe: ded@arushadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.