• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe |
Arusha District Council
Arusha District Council

Serikali ya jamuhuri ya Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili Makuu
    • Mikkati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara na Vitengo
      • Utawala na Utumishi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Fadha na Biashara
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliji
      • Ardhi na Maliasili
      • Maji
      • Works
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo na Umwagiliaji na Ushirika
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Internal Audit
      • Nyuki
      • Uchaguzi
      • UKIMWI/ AIDS
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Livestock
    • Wadau wa Maendeleo
  • Huduma Zetu
    • Health
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Utawala Fedha na Mipango
      • Elimu Afya na Maji
      • Kudhibiti UKIMWI
      • Maadili ya Madiwani
      • Uchumi Ujenzi na Mazingira
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Vikao vya Timu ya Uendeshji ya Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mktaba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa UMMA
    • Video za Shoghuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

Arusha DC kuchele, wapata msaada wa magari matano kutoka Kikundi cha Friends of German

Posted on: November 14th, 2018

Ule msemo usemao 'Mgeni njoo mwenyeji apone' umedhirika dhahiri ndani ya halmashauri ya Arusha wilayani Arumeru, baada ya Shirika lisilo la kiserikali la Help for Maasai Childreni (HMC), kwa kushirikiana na wafadhili wa Kundi la Friends of German la nchini Ujerumani, kutoa msaada wa magari matano kwa lengo la kutatua changamoto zinazoikabili jamii.

Wananchi wa halmashauri hiyo, walishindwa kuficha hisia zao kwa kucheza na kuimba, mara baada ya magari hayo kuwasili katika halmashauri hiyo hususani wananchi wa kata ya Oldonyowas ambao ndio wanufaika wakubwa wa msaada huo.

Akipokea msaada huo Mkuu wa wilaya ya Arumeru mhe. Jerry Muro amewashukuru wafadhili hao kwa msaada huo wenye tija kwa wananchi wa halmashauri ya Arusha na wilaya ya Arumeru kwa ujumla wake, pamoja na kumpongeza Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo  Dkt. Wilson Mahera  kwa kushirikiana vyema na Taasisi hizo na kuweza kuchangishana fedha za kununua magari hayo kutoka nchini Ujerumani na  hatimaye msaada huo kuwafikia wananchi wa Arumeru.

Aidha Mkuu huyo wa Wilaya amepongeza juhudi kubwa, zinazoendelea kufanywa na Taasisi hizo, katika kutekeleza miradi ya huduma za jamii katika, sekta nyeti za  Elimu, Afya na Maji, na kuwawezesha, wananchi wa Oldonyowas kupata huduma muhimu ndani ya eneo lao ambapo hapo awali ilikuwa inawawia ugumu kupata huduma hizo.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya Arusha Dkt. Wilson Mahera, amewaelezea wafadhili kuwa, waliingia hapa nchini mwaka 2005, na wamekuwa wakifadhili utekelezaji wa miradi ya maji, elimu na afya kwenye kata za Oldonyosambu na Oldonyowasi.

Amefafanua kuwa halmashauri hiyo, imepokea jumla ya magari matano, kati ya hayo, magari mawili ni ya kubeba wagonjwa 'Ambulance' ambayo ni 'mobile clinic' yakiwa na vifaa muhimu vya kuweza, kufanyia mgonjwa upasuaji ndani ya gari, na kuongeza kuwa magari matatu aina ya 'Pick up' yatatumika kwa shughuli mbalimbali ndani ya halmashauri hiyo.

Hata hivyo alieleza kuwa, mwaka 2009, wafadhilia hao walitekeleza mradi wa Afya kwa kujenga Zahanati ya kisasa katika kata ya Oldoyowasi, ambayo imejitosheleza kwa vifaa tiba, Zahanati ambayo imewapunguzia adha wananchi wa Oldonyowas ya kutembea umbali mrefu kutafuta huduma ya afya.

Dkt. Mahera amesisitiza kuwa, wafadhili hao ni muhimu kwa halmshauri yake, kwa kuwa tayari wamejenga jumla ya shule saba za awali sambamba na kuwapeleka waalimu kwenye mafunzo ya ualimu kwa lengo la kufundisha watoto wa madarasa hayo ya awali.

Mkurugenzi wa shirika la Help for Masaai Childreni, Joseph Kivuyo licha ya kushukuru kwa msaada huo, ameeleza kuwa, lengo la kutolewa magari hayo ni kurahisisha kutoa huduma kwa wananchi waishio katika maeneo yenye mazingira magumu hususani vijijini.

“Tuliamua kuchanga fedha za kununua magari haya kutokana na jamii inayotuzunguka kuwa na uhitaji mkubwa wa uhudama hii hasa wanawake ambao mara nyingi ndiyo waliokuwa wakitembea umbali wa kilomita 18 kwenda kwenye vituo vya mbali kutafuta huduma,” amesema Kivuyo.

Naye kiongozi wa kundi la Friends of German, ambaye ndiye mfadhili aliyechangisha fedha za kununua magari hayo, Harld Ppeiffer, amesema kuwa, miaka kumi iliyopita alipata wazo la kuja katika nchi za bara la Afrika kwa ajili ya kusaidia watoto kupata elimu.

Amedai kuwa, kutoa elimu bora kwa watato ni jambo muhimu sana, kwa sababu itawafanya kuwa na malengo mazuri kwa maisha yao ya baadae na kuongeza kuwa,  msaada huo wa magari ni muhimu katika kutimiza wazo lake la kuwasaidia watoto wa Afrika hasa nchini Tanzania na watoto wa kata ya Oldonyowas.

Ppeiffer amefafanua kuwa, kupitia safari hiyo ya kuleta magari hayo, wanategemea kukusanya fedha kiasi cha 'Euro 300,000, fedha ambazo zitakazotumika kwenye ujenzi wa Kituo cha Afya Oldonyowas iliyopo kata ya Oldonyowas na kiasi kingine kutumika katika shughuli nyingine za Idara ya Afya.

Awali mchakato wa kuyaleta magari hayo, umetumia muda wa wiki saba  kwa kuyasafirisha kwa kupitia nchi kavu, kutokea nchini Ujerumani na kupitia nchi za Misri, Ethiopia, Kenya na hatimaye kuwasili nchini Tanzania hususani halmashauri ya Arusha wilayani Arumeru.

PICHA ZA MAGARI YALIYOTOLEWA MSAADA KWA HALMASHAURI YA ARUSHA.



Magari aina ya 'Pick Up' kwa ajili ya shughuli mbalimbali za halmashauri


Gari la kububea wagonjwa wa dharura 'Ambulance'




Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA MKATABA ENABOISHU FM - ARUSHA DC May 26, 2025
  • ORODHA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO 2023 ARUSHA DC June 11, 2023
  • ZIARA YA WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS TAMISEMI, MHE. MOHAMED O. MCHENGERWA 17 SEPTEMBA 2024 September 13, 2024
  • MTIHANI WA DARASA LA SABA 11-12/09/2024 September 09, 2024
  • Tazama zote

Habari mpya

  • VIONGOZI WA DINI WAPEWA ELIMU YA CHAKULA BORA

    May 28, 2025
  • VIONGOZI WA DINI WAPEWA ELIMU YA AFYA YA MAMA NA MTOTO

    May 27, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA MKATABA

    May 26, 2025
  • RC MAKONDA ATEMBELEA NA KUKAGUA MRADI WA UJENZI WA MAHAKAMA YA AFRIKA ARUSHA

    May 25, 2025
  • Tazama zote

Video

Video zaidi

Viunganishi vinavyoingiliana

  • Leseni ya vileo
  • Fomu ya ukaguzi

Viunganishi vinavyohusiana

  • Tovuti kuu ya serikali
  • Tamisemi
  • Utumishi portal
  • Wakala wa serikali mtandao
  • Mkoa wa arusha
  • ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Sekei Road

    Anuani ya posta: 2330 Arusha

    Simu : +255 027 2502737

    Simu: 073 65000476

    Barua pepe: ded@arushadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.