Na. Elinipa Lupembe
Uongozi wa halmashauri ya Arusha, umeungana na watanzania wote nchini, kuadhimisha miaka 58 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, kwa kufanya shughuli za ujenzi, kwenye shule mpya ya sekondari kata ya Kiutu, shule inayojengwa na serikali kupitia miradi ya SEQUIP huku wananchi wakichangia nguvu kazi, kukamilisha ujenzi huo.
Uongozi huo wa halmashauri ya Arusha, uliowajumuisha Mwenyekiti wa halmashauri ya Arusha, Mhe. Ojung'u Salekwa, Mbunge wa Jimbo la Arumeru Magharibi Mhe. Noah Lembris, Diwani wa kata ya Kiutu Mhe. Malaki Malambo, na Diwani wa Viti Maalum Mhe. Nina Masanja pamoja na watalamu wa kuanzia ngazi ya halmashauri, kata hadi vijiji wakingozwa na Mkurugenzi Mtendaji, Halmashauri ya Arusha, Seleman Msumi.Uongozi huo, umefikia hatua hiyo, ikiwa ni utekelezaji wa magizo ya Serikali ya kila halmashauri kufanya maadhimisho ya Sikukuu ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar katika maeneo yao kwa kufanya shughuli za kijamii, ikiwa ni kuamsha Ari kwa wananchi kufanya kazi kwa maendeleo yao na Taifa kwa ujumla.
*MUUNGANO NI TUNU YETU, NI WAJIBU WETU WATANZANIA KUUENZI*✍✍
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.