• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe |
Arusha District Council
Arusha District Council

Serikali ya jamuhuri ya Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili Makuu
    • Mikkati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara na Vitengo
      • Utawala na Utumishi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Fadha na Biashara
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliji
      • Ardhi na Maliasili
      • Maji
      • Works
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo na Umwagiliaji na Ushirika
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Internal Audit
      • Nyuki
      • Uchaguzi
      • UKIMWI/ AIDS
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Livestock
    • Wadau wa Maendeleo
  • Huduma Zetu
    • Health
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Utawala Fedha na Mipango
      • Elimu Afya na Maji
      • Kudhibiti UKIMWI
      • Maadili ya Madiwani
      • Uchumi Ujenzi na Mazingira
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Vikao vya Timu ya Uendeshji ya Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mktaba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa UMMA
    • Video za Shoghuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

ARUSHA DC YAWAPONGEZA WAKULIMA WALIOISABABISHIA USHINDI WA KWANZA NANENANE 2020

Posted on: August 14th, 2020

Na. Elinipa Lupembe.

   Halmashari ya Arusha imeendelea kusherehekea ushindi wa kwanza uliopatikanaa kwenye kilele cha sherehe za Nanenane, kwa kuwakabidhi zawadi  za pongezi Wakulima na Wafugaji waliofanikisha  halmashauri hiyo kuibuka kidedea, kwa kushika nafasi ya kwanza kwa Mifugo na Mazao kwa halmashauri za mikoa ya Arusha, Kilimanjaro na Manyara, kwenye maonyesho ya nanenane Kanda ya Kaskazini 2020

      Akikabidhi zawadi hizo Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Arusha, Saad Mtambule, kwenye hafla fupi iliyofanyika kwenye ofisi za halmashauri hiyo, licha ya kuwapongeza washiriki hao, amethibitisha kuwa ushindi huo wa halmashauri umetokana na juhudi za wakulima na wafugaji hao.

   Ameongeza kuwa, halmashauri inapata urahisi wa kutekeleza majukumu yake, pale ambapo wananchi wake wanaonesha juhudi za kuiunga mkono pamoja na kutumia vyema fursa na huduma zinazotolewa na halmashauri yao.                                                                                                                                                                                 "Tunajivunia kuwa nanyi wananchi wetu, sisi kama Halmashauri bila nyinyi wananchi, hususani wakulima na wafugaji, hatuwezi kutekeleza majukumu yetu wala mipango ya Serikali, lakini uwepo wenu na ushiriki wenu kwenye shughuli za serikali unaleta tija kwa maendeleo ya Taifa letu"amesema Mtambule.

      Ameendelea kuwataka wakulima na wafugaji hao, kutumia fursa, utalamu na teknolojia za kisasa ili kufanya mapinduzi kwenye sekta ya kilimo na mifugo kwa kuzalisha mazao yenye ubora pamoja na kutumia mnyororo wa thamani katika uzalishaji huo, kwa kuongeza thamani mazao yanayoyazalisha.

      Hata hivyo Mkurugenzi Mtambule, amesema kuwa, licha ya wakulima na wafugaji kuanza kutumia teknolojia za kisasa na kufanya kilimo biashara lakini bado kuna changamoto ya utengenezaji wa bidhaa za mazao ya mifugo na kilimo zenye ubora pamoja na ushindani mkubwa wa masoko ya wazi.

    Aidha ameweka wazi kuwa halmashauri ina mkakati wa kuanzisha eneo maalum kwa ajili ya wajasiriamali kuweka bidhaa zao, kwa lengo la kuwakutanisha pamoja awajasiriamali wa halmashauri hiyo, lengo likiwa kurahisha upatikanaji wajasiriamali hao, kuonyesha bidhaa na kupata masoko katika eneo moja.

     "Halmashauri iko kwenye mazungumzo na wadau ambao wameonesha nia ya kuwekeza kweye eneo ambalo, litakuwa 'industrial area' ambapo wajasiriamali wa sekta zote watakaa hapo kwa ajili ya kutengeneza bidhaa zao na  eneo ambalo litakuwa ni soko la pamoja la kuonesha na na kuuza bidhaa hizo, hivyo niwatake wajasiriamali kuitumia fursa hiyo pindi itakapokuwa tayari"ameweka wazi Mkurugenzi huyo.

    Jumla ya washiriki 6  walioshika nafasi tatu za mwanzo wamepatiwa fedha taslimu, ikiwa ni wafugaji watatu na wakulima watatu, na walishiriki wote wamepewa vyeti vya pongezi kwa ushiriki na kutakiwa kutolukata tamaa  na kuendelea kujipanga kwa ajili ya maonesho ya mwaka ujao.

   Hata hivyo wakulima hao, wameipongeza na kuishukuru halmashauri kwa kuwajali, kwa watalamu kuwafuata kwenye maeneo yao kwa kuwapa huduma za kitalamu, zinazowawezesha wakulima kufanya uzalishaji wenye tija na kupata mazao bora.

     John Alfayo, ameomba kama halmashauri kuwa na maonesho ya wakulima na wafugaji  yatakayo wakutanisha wote ili kufahamiana na  kupata fursa ya kubadilishana uzoefu.

     Maadhimisho ya nane nane hufanyika kila mwaka ambapo Kanda ya Kasikazini hufanyika kwenye viwanjwa vya Themi eneo la  Njiro  jijini Arusha.


PICHA ZA MATUKIO









Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA MKATABA ENABOISHU FM - ARUSHA DC May 26, 2025
  • ORODHA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO 2023 ARUSHA DC June 11, 2023
  • ZIARA YA WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS TAMISEMI, MHE. MOHAMED O. MCHENGERWA 17 SEPTEMBA 2024 September 13, 2024
  • MTIHANI WA DARASA LA SABA 11-12/09/2024 September 09, 2024
  • Tazama zote

Habari mpya

  • VIONGOZI WA DINI WAPEWA ELIMU YA CHAKULA BORA

    May 28, 2025
  • VIONGOZI WA DINI WAPEWA ELIMU YA AFYA YA MAMA NA MTOTO

    May 27, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA MKATABA

    May 26, 2025
  • RC MAKONDA ATEMBELEA NA KUKAGUA MRADI WA UJENZI WA MAHAKAMA YA AFRIKA ARUSHA

    May 25, 2025
  • Tazama zote

Video

Video zaidi

Viunganishi vinavyoingiliana

  • Leseni ya vileo
  • Fomu ya ukaguzi

Viunganishi vinavyohusiana

  • Tovuti kuu ya serikali
  • Tamisemi
  • Utumishi portal
  • Wakala wa serikali mtandao
  • Mkoa wa arusha
  • ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Sekei Road

    Anuani ya posta: 2330 Arusha

    Simu : +255 027 2502737

    Simu: 073 65000476

    Barua pepe: ded@arushadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.