Na. Elinipa Lupembe.
Halmashauri ya Arusha imeungana na watu wote duniani, kuadhimisha Siku ya Usafishaji Mazingira Duniani kwa kujiimarisha katika usafishaji na utunzaji wa mazingira katika maeneo yote ya mito na vyanzo vya maji.
Katika maadhimisho hayo, Kaimu Mkurugenzi, halmashauri hiyo, amewaongoza wananchi waishio kata ya Kiranyi hususani wale wa pembezoni mwa Mto Ngarenaro kusafisha na kuondoa taka kwenye kingo za mto huo, zoezi lilochukua takribani saa 5.
Akizungumza baada ya kukamilika kwa zoezi hilo, Kaimu Mkurugenzi halmashauri ya Arusha ambaye ni Mkuu wa Kitengo cha Sheria, Wakili msomi Monica Mwailolo, amewataka wananchi wote kuhakikisha wanaendelea kutunza maeneo ya mito sambamba na utunzaji wa vyanzo vya maji, lengo likiwa ni kuweka uso wa dunia safi kwa hewa safi na afya za watu na viumbe vyote.
"Niwatake wananchi wote, zoezi la kusafisha mito liwe endelevu na kuhakikisha kila kijiji na kitongoji kinakuwa na sheria za kuwabana wachafuzi wa mazingira sambamba na kumchukulia hatua kali, mtu yoyote atakayechafua mazingira kwa makusudi atozwe faini kulingana na sheria husika". Amesisitiza Kaimu Mkurugenzi huyo
Hata hivyo wananchi wa kitongoji cha Ilkiurei, wameupongeza uongozi wa halmashauri hiyo kwa kuchagua eneo lao, kuadhimisha siku hiyo muhimu ya kidunia na kuahidi kuendelea kusafisha na kutunza kingo za mto Ngarenare na maeneo ya vyanzo vya maji.
Diwani wa kata ya Kiranyi, Mhe. John Seneu amesema kuwa, tayari kata ya Kiranyi na vitongoji vyake, imejipanga kufanya mikutano ya vitongoji ili kuwasisitiza wananchi mikakati ya usafishaji na utunzaji wa kingo za mto Ngarenaro na vyanzo vya maji.
Naye Mkuu wa kitengo cha Usafishaji, Halmashauri ya Arusha, Zuraika kundya, amesema kuwa zoezi la usafi wa mazingira ni zoezi endelevu katika maeneo yote ya halmashauri hiyo na kuwataka wananchi wote, kuhakikisha wanasafisha maeneo yao bila kulazimishwa wala kushurutishwa na sheria.
Ameitaja siku ya Usafishaji mazingira Duniani kuwa ni siku muhimu kwa afya za binadamu na viumbe vyake, hivyo ushiriki wa kila mmoja kuiweka uso wa dunia safi ni wa muhimu kwa vizazi na vizazi.
Maadhimisho ya siku ya Usafishaji Mazingira duniani yenye Kauli Mbiu ya "Ondoa Takataka na Taka sizizodhibitiwa kutoka kwenye Vyanzo vya Maji", imafanyika kwa mafanikio makubwa huku watu wote duniani wakishiriki kuiweka dunia safi.
ARUSHA DC
TUPO KAZINI✍✍
PICHA ZA MATUKIO WAKATI WA ZOEZI LA USAFI
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.