• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe |
Arusha District Council
Arusha District Council

Serikali ya jamuhuri ya Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili Makuu
    • Mikkati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara na Vitengo
      • Utawala na Utumishi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Fadha na Biashara
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliji
      • Ardhi na Maliasili
      • Maji
      • Works
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo na Umwagiliaji na Ushirika
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Internal Audit
      • Nyuki
      • Uchaguzi
      • UKIMWI/ AIDS
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Livestock
    • Wadau wa Maendeleo
  • Huduma Zetu
    • Health
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Utawala Fedha na Mipango
      • Elimu Afya na Maji
      • Kudhibiti UKIMWI
      • Maadili ya Madiwani
      • Uchumi Ujenzi na Mazingira
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Vikao vya Timu ya Uendeshji ya Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mktaba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa UMMA
    • Video za Shoghuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

ARUSHA DC YAANZA MKAKATI WA KUTHIBITI MINYOO YA TUMBO KWA WATOTOWA MIAKA 5- 14

Posted on: November 11th, 2022

Na Elinipa Lupembe

Halmashauri ya Arusha, imeanza mkakati wa kutekeleza mpango jumuishi wa Taifa wa kudhibiti Magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele, kwa watoto wenye umri wa kuanzia miaka 5 mpaka 14, walioandikishwa shule na wasio kwenye mfumo wa shule.

Akizungumza wakati wa kikao kazi hicho, Katibu Tawala wilaya ya Arumeru, Mwl. James Mchembe, ameitaka timu ya watalamu iliyoteuliwa kuhakikisha wanafanya kazi hiyo kwa bidii na kwa kushirikiana ili kufikia malengo yaliyokusudiwa.

"Huu ni mpango wa kitaifa, tunatakiwa kuhakikisha tunatekeleza shughuli hii kila mmoja kwa nafasi yake, ili kufikia malengo ya serikali ya kuwakinga watoto ambao wako kwenye hatari kubwa ya kuambukizwa magonjwa ya minyoo tumbo ili kuwaandaa watoto kuwa na Taifa lenye watu wenye afya bora hapo baadaye". Amesisitiza Katibu Tawala huyo.

Aidha Katibu Tawala huyo, amewataka watalamu licha ya kutoa dawa kinga hizo, ni vema kujikita pia kutoa elimu ya usafi kwa jamii, ili kujikinga na minyoo kwa kuwa na vyoo bora pamoja na kuwa na tabia chanya za afya za kunawa mikono kwa maji safi na sabuni kabla ya kula, kabla ya kunyonyesha mtoto, wakati wa kumtawaza mtoto na mara  baada ya kutoka chooni pamoja na watoto kuvalishwa viatu.

Hata hivyo Mwenyekiti wa Halmashauri ya Arusha, mhe. Ojung'u Salekwa, ameishukuru serikali kwa mpango huo mpango ambao una manufaa makubwa kwa watoto, wananchi na jamii kwa ujumla wake.

"Ninaipongeza serikali, ninamshukuru mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan, kwa kuwa na mpango wa  kuandaa watoto wenye afya bora, watoto ambao ni wajenzi wa Taifa la kesho, mtoto asiyeshambuliwa na magonjwa afya yake ya akili inayomuwezesha mtoto kulitumikia taifa lake akiwa na afya bora" Amesisitiza Mwenyekiti Ojung'u

Mganga mkuu halmashauri ya Arusha, Dkt. Peter Mboya, ameweka wazi kuwa, halmashauri inategemea kutoa kinga tiba ya minyoo tumbo kwa watoto 80,000 wa kuanzia miaka 5 mpaka 14, walio kwenye mfumo wa shuleni na wasio kwenye mfumo wa shule.

Amefafanua kuwa makusudi ya mpango ni kuendeleza mpango jumuishi wa Taifa wa kudhibiti magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele ukiwa na dira ya kuwa na jamii yenye afya bora na ustawi na usiyodhoofisha na madhara ya magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele.

Mratibu wa magonjwa yasiyo ya kuambukizwa halmashauri ya Arusha, Ramadhani Kulewa, amesema kuwa halmashauri inategemea kutoa kinga tiba ya ugonjwa wa minyoo tumbo kupitia vituo 211, vituo vya afya 56 na kwenye shule za msingi 155 huku wahudumu 433 wakiwemi walimu 310 na wahudumu wa afya 112.

Kulewa aethibitisha kuwa ili kufikia lengo, licha ya kuwa na vituo hivyo maalum halmashauri pia itatumia mfumo wa ugawaji dawa katika jamii kwa kupita nyumba kwa nyumba, ugawaji wa dawa kwa makundi maalum, pamoja na kwenye mikusanyiko ya watu kama nyumba za ibada, sokoni, vituo vya mabasi na meeneo yote ya biashara.

Awali halmashauri ya Arusha inategemea kuwapatia kinga tiba ya minyoo kwa watoto 80,000, watoto 76,000 kati yao ni wale waliosajiliwa shuleni na watoto 4,000 ni ambao hawajasajiliwa kwenye mfumo rasmi wa elimu.

ARUSHA DC

KaziInaendelea 





Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA MKATABA ENABOISHU FM - ARUSHA DC May 26, 2025
  • ORODHA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO 2023 ARUSHA DC June 11, 2023
  • ZIARA YA WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS TAMISEMI, MHE. MOHAMED O. MCHENGERWA 17 SEPTEMBA 2024 September 13, 2024
  • MTIHANI WA DARASA LA SABA 11-12/09/2024 September 09, 2024
  • Tazama zote

Habari mpya

  • VIONGOZI WA DINI WAPEWA ELIMU YA CHAKULA BORA

    May 28, 2025
  • VIONGOZI WA DINI WAPEWA ELIMU YA AFYA YA MAMA NA MTOTO

    May 27, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA MKATABA

    May 26, 2025
  • RC MAKONDA ATEMBELEA NA KUKAGUA MRADI WA UJENZI WA MAHAKAMA YA AFRIKA ARUSHA

    May 25, 2025
  • Tazama zote

Video

Video zaidi

Viunganishi vinavyoingiliana

  • Leseni ya vileo
  • Fomu ya ukaguzi

Viunganishi vinavyohusiana

  • Tovuti kuu ya serikali
  • Tamisemi
  • Utumishi portal
  • Wakala wa serikali mtandao
  • Mkoa wa arusha
  • ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Sekei Road

    Anuani ya posta: 2330 Arusha

    Simu : +255 027 2502737

    Simu: 073 65000476

    Barua pepe: ded@arushadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.