Na. Elinipa Lupembe.
Halmashauri ya Arusha imeendelea kung'ara kitaaluma kwa kufanikisha, shule zake mbili za serikali kuingia kwenye nafasi 10 bora kitaifa, kwa mujibu ya matokeo ya kidato cha sita, yaliyotangazwa leo na BARAZA LA MITIHANI LA TAIFA - NECTA.
Akizungumza ofisini kwake mkurugenzi mtendaji halmashauri ya Arusha, Saad Mtambule, amezitaja shule hizo ni shule ya sekondari Ilboru iliyoshika nafasi ya 8 na Shule sekondari Mwandeti iliyoshika nafasi ya 9, na kufanya shule mbili kuingia kwenye nafasi 10 bora.
Aidha amewapongeza watalamu, walimu, wanafunzi na wadau wote wa elimu, halmashauri ya Arusha, kwa pamoja kuwezesha shule hizo kuafanya vizuri katika mitihani ya taifa 2020
BOFYA LINK HII KUPATA MATOKEO YA KIDATO CHA SITA,2020........https://matokeo.necta.go.tz/acsee/index.htm
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.