• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe |
Arusha District Council
Arusha District Council

Serikali ya jamuhuri ya Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili Makuu
    • Mikkati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara na Vitengo
      • Utawala na Utumishi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Fadha na Biashara
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliji
      • Ardhi na Maliasili
      • Maji
      • Works
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo na Umwagiliaji na Ushirika
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Internal Audit
      • Nyuki
      • Uchaguzi
      • UKIMWI/ AIDS
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Livestock
    • Wadau wa Maendeleo
  • Huduma Zetu
    • Health
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Utawala Fedha na Mipango
      • Elimu Afya na Maji
      • Kudhibiti UKIMWI
      • Maadili ya Madiwani
      • Uchumi Ujenzi na Mazingira
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Vikao vya Timu ya Uendeshji ya Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mktaba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa UMMA
    • Video za Shoghuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

Arusha DC yajipanga kuboresha uzalishaji wa ng'ombe bora wa maziwa

Posted on: April 18th, 2018

Halmashauri ya Arusha kupitia Idara ya Mifugo imejipanga kuboresha uzalishaji wa ng'ombe bora wa maziwa kwa kutoa mafunzo kwa wafugaji ndani ya halmashauri.

Mikakati hiyo inafuatia teknolojia ya uhamilishaji safu za koo za ng'ombe wa maziwa 'artificial insemination', zoezi lililoanza kufanyika mapema mwaka uliopita, 2017.               

Akizungumza wakati wa mafunzo hayo, Daktari wa Mifugo, halmashauri ya Arusha Dkt. Yohana Kiwone amesema kuwa, lengo la kutoa mafunzo hayo ni kuwafanya wafugaji kuhama kutoka ufugaji wa mazoea usio na faida na kuanza ufugaji wa kisasa unaowapeleka wafugaji, kwenye uzalishaji wa kibiashara.                  

Dkt. Kiwone ameelezea umuhimu wa uhamilishaji ni koboresha safu za koo za ng'ombe, kwa kumpandikiza ng'ombe mbegu bora yenye nyama na maziwa mengi kwa kufuga ng'ombe wachache kwenye eneo dogo.             

Ameongeza kuwa, licha ya telnolojia ya uhimilishaji kuimarisha ufugaji kwa kuwa na ng'ombe bora,  teknolojia hii inakwenda sambamba na utunzaji wa mazingira. 

Aidha Dkt Kiwone amethibitisha kuwa, kupitia mafunzo hayo mfugaji anajengewa uwezo wa kufahamu vizuri mbegu na koo ya ng'ombe anayemfuga  pamoja na kuwa na kumbukumbu, zenye taarifa sahihi za ng'ombe wake.   

 "Wafugaji wengi wanafuga ng'ombe bila hata kufahamu aina wala ukoo wa ng'ombe anayemfuga, wala kuwa na taarifa na kumbukumbu sahihi za ng'ombe wake jambo lililokuwa linawafanya wafugaji kufuga kwa mazooea na kuendelea kuwa masikini" amesema Daktari huyo.      

Hata hivyo, Wafugaji wamefurahia mafunzo hayo, kwa kusema kuwa wameanza kupata mwanga wa mafanikio kupitia mifugo ambayo awali, wamekua wakifuga kwa mazoea bila kuwa na utalamu wowote.       

Wafugaji hao wamekiri mifugo yao inawapa chakula tuu na si zaidi ya hapo licha ya gharama kubwa wanazotumia kuhudumia ng'ombe hao.     

Naishiye Laizer mkazi wa Losikito amethibitisha kuwa, wafugaji wengi katika maeneo yao hupata kiasi kidogo cha maziwa kinachotumika kwa familia na kuuza kiasi kidogo sana.    

" Mifugo yetu  inatupatia maziwa ya kunywa watoto nyumbani, kama ni kuuza tunauza maziwa kidogo lita moja au mbili,wakati tunatumia nguvu nyingi na uzalishaji ni mdogo kabisa" amesema Naishiye.      

Hata hivyo Naishiye amekiri kuwa, mafunzo hayo yamewafungua macho na kuwapa mwanga wa matunda bora, yanayoweza kupatikana kupitia ufugaji bora hasa kupitia utalamu wa  uhamilishaji.     

Awali Dkt. Kiwone amefafanua kuwa halmashauri imepanga kutoa mafunzo kwa wafugaji 900 kwa awamu ya ya kwanza mpaka kufikia mwezi Agosti mwaka 2018 na mpaka jumla ya wafugaji 427 wameshafikiwa ndani ya vijiji na  vitongoji vya Mamlaka ya mji mdogo Ngaramtoni.

Matangazo

  • TANGAZO LA KAZI ZA MKATABA HALMASHAURI YA WILAYA YA ARUSHA August 14, 2025
  • ORODHA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO 2023 ARUSHA DC June 11, 2023
  • ZIARA YA WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS TAMISEMI, MHE. MOHAMED O. MCHENGERWA 17 SEPTEMBA 2024 September 13, 2024
  • MTIHANI WA DARASA LA SABA 11-12/09/2024 September 09, 2024
  • Tazama zote

Habari mpya

  • KUFUATILIA NA USAMIZI WA HAKI ZA MTOTO KATIKA JAMII NI JAMBO MUHIMU

    August 25, 2025
  • RAIS SAMIA AMUAPISHA AMOS MAKALLA KUWA MKUU WA MKOA WA ARUSHA

    August 26, 2025
  • DKT. JAHANNES LEMBULUNG' LUKUMAY ACHUKUWA FOMU YA UGOMBEA UBUNGE WA CCM JIMBO LA ARUMERU MAGHARIBI

    August 25, 2025
  • KIKAO KAZI CHA WENYEVYITI WA BODI NA WATENDAJI WAKUU WA TAASISI ZA UMMA (CEOs Forum 2025)

    August 24, 2025
  • Tazama zote

Video

Video zaidi

Viunganishi vinavyoingiliana

  • Leseni ya vileo
  • Fomu ya ukaguzi

Viunganishi vinavyohusiana

  • Tovuti kuu ya serikali
  • Tamisemi
  • Utumishi portal
  • Wakala wa serikali mtandao
  • Mkoa wa arusha
  • ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Sekei Road

    Anuani ya posta: 2330 Arusha

    Simu : +255 027 2502737

    Simu: 073 65000476

    Barua pepe: ded@arushadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.