• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe |
Arusha District Council
Arusha District Council

Serikali ya jamuhuri ya Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili Makuu
    • Mikkati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara na Vitengo
      • Utawala na Utumishi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Fadha na Biashara
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliji
      • Ardhi na Maliasili
      • Maji
      • Works
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo na Umwagiliaji na Ushirika
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Internal Audit
      • Nyuki
      • Uchaguzi
      • UKIMWI/ AIDS
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Livestock
    • Wadau wa Maendeleo
  • Huduma Zetu
    • Health
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Utawala Fedha na Mipango
      • Elimu Afya na Maji
      • Kudhibiti UKIMWI
      • Maadili ya Madiwani
      • Uchumi Ujenzi na Mazingira
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Vikao vya Timu ya Uendeshji ya Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mktaba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa UMMA
    • Video za Shoghuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

ARUSHA DC YANG'ARA MASHINDANO YA UMISETA MKOA WA ARUSHA

Posted on: August 4th, 2022

Na Elinipa Lupembe

Halmashauri ya Arusha imeendelea kung'ara katika mashindano ya michezo shule za sekondari UMISETA ngazi ya mkoa, kwa kuchukua jumla ya makombe manne, medali 6 za dhahabu, 3 za shaba na 1 ya fedha, huku wachezaji 20, wakichaguliwa kuwakilisha mkoa ngazi ya Taifa, mashindano yanayotegemea kufanyika mkoani Tabora.

Wakizungumza wakati wa kukabidhi makombe hayo kwa mkurugenzi Mtendaji halmashauri ya Arusha, Seleman Msumi, kwenye ofisi za makao makuu ya halmashauri hiyo, wachezaji hao wamesema siri kubwa ya ushindi ni nidhamu na kufuata maelekezo ya makocha katika michezo.

Damian Christian mmoja wa wanariadha aliyeshinda medali ya dhahabu, amekiri siri kubwa ya mafanikio katika timu zao, ni kuwa na malengo, juhudi binafsi, nidhamu, ushirikiano pamoja na kufuata maelekezo ya walimu wao wakati wote wa michezo wakiwa  kambini.

"Sisi kama wachezaji, tuliingia kwenye mashindano tukiwa na malengo ya ushindi, tukaweka juhudi na nidhamu, kwa pamoja zikatuwezesha kufikia lengo la ushindi na kupata makombe na medali hizi" Amesisitiza mwanariadha Damian.

Hata hivyo Mkurungenzi Msumi, licha ya kuwapongeza kwa ushindi huo mnene, ameonyesha kufurahishwa na uwakilishi mzuri wa wachezi hao kwa kuiwakilisha vema halmasahuri yao na kurudi na makombe na medali.

Aidha amewapongeza wachezaji 20 waliochaguliwa kuwakilisha mkoa ngazi ya Taifa, na kuwataka kuongeza bidii na nidhamu zaidi pamoja na kufuatilia maelekezo na mbinu za wanaozofundishwa na walimu, na kuwasisitiza kurudi na ushindi kama ilivyokuwa katika ngazi ya mkoa.

"Nidhamu ndio kila kitu, hivyo ninawaamini vijana wangu nendeni mkapambane kwa manufaa ya halmashauri yetu, mkoa wa Arusha pamoja na Taifa kwa ujumla, mnafahamu michezo ni ajira, hivyo jitahidini ili vipaji mlivyonavyo viweze kuwafikisha mbali zaidi katika kulitumika Taifa la Tanzania". Amesisitiza Mkurugenzi Msumi.

Naye Afisa Elimu Sekondari halmashauri ya Arusha, Mwl. Menard Lupenza amefafanua kuwa katika mashindano ya UMISETA ngazi ya mkoa, halmashauri ya Arusha ilipata ushindi wa kwanza kwenye michezo mitatu ya soka la wasichana, mpira wa Pete na wasanii wa kizazi kipya, ushindi wa pili kwenye Mpira wa wavu kwa wavulana na riadha wavulana, ushindi wa tatu Fani za ndani ngoma na kwaya, mpira wa kikapu wavulana na wasichana na mpira wa mikono kwa wavulana.

Ameongeza kuwa kwa matokeo ya jumla halmashauri imeshika nafasi ya nne na kufanikiwa kupata jumla ya makombe 4, medali 6 za dhahabu, 3 za shaba na 1 moja ya fedha, huku jumla ya wanamichezo 20 wakichaguliwa kuwakilisha mkoa kwenye mashindano ya UMISETA ngazi ya Taifa yenye Kauli mbiu ya "TAKWIMU SAHIHI NI MSINGI WA MIPANGO BORA YA TAIFA" SHIRIKI SENSA YA WATU NA MAKAZI KWA MAENDELEO YETU" .


SHIRIKI SENSA YA WATU NA MAKAZI 2022

JIANDAE KUHESABIWA ✍✍



Mkurugenzi Mtendaji halmashauri ya Arusha, seleman Msumi, akiwa ameshikilia makombe na medali za ushindi wa UMISETA ngazi ya mkoa, mara baada ya kukabidhiwa na wachezaji 20 waliochaguliwa kujiunga na timu ya mkoa wa Arusha kushiriki UMISETA ngazi ya Taifa.





Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA MKATABA ENABOISHU FM - ARUSHA DC May 26, 2025
  • ORODHA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO 2023 ARUSHA DC June 11, 2023
  • ZIARA YA WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS TAMISEMI, MHE. MOHAMED O. MCHENGERWA 17 SEPTEMBA 2024 September 13, 2024
  • MTIHANI WA DARASA LA SABA 11-12/09/2024 September 09, 2024
  • Tazama zote

Habari mpya

  • VIONGOZI WA DINI WAPEWA ELIMU YA CHAKULA BORA

    May 28, 2025
  • VIONGOZI WA DINI WAPEWA ELIMU YA AFYA YA MAMA NA MTOTO

    May 27, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA MKATABA

    May 26, 2025
  • RC MAKONDA ATEMBELEA NA KUKAGUA MRADI WA UJENZI WA MAHAKAMA YA AFRIKA ARUSHA

    May 25, 2025
  • Tazama zote

Video

Video zaidi

Viunganishi vinavyoingiliana

  • Leseni ya vileo
  • Fomu ya ukaguzi

Viunganishi vinavyohusiana

  • Tovuti kuu ya serikali
  • Tamisemi
  • Utumishi portal
  • Wakala wa serikali mtandao
  • Mkoa wa arusha
  • ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Sekei Road

    Anuani ya posta: 2330 Arusha

    Simu : +255 027 2502737

    Simu: 073 65000476

    Barua pepe: ded@arushadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.