Na. Elinipa Lupembe.
Hayawi hayawi sasa yamekuwa, halmashauri ya Arusha imeng'ara kwenye Tuzo za Ubora wa Taaluma, katika matokeo ya Mtihani wa kumaliza Elimu ya Msingi, Kidato cha Nne na Kidato cha sita mwaka 2021, kwa kuwa halmashauri ya pili kitaifa na ya kwanza kwa shule za serikali, tuzo zilizolotewa leo kwenye ukumbi wa chuo cha Biblia Jijini Dodoma.
Katika Tuzo hilo maalum, halmashauri ya Arusha imefanikiwa kupata cheti na Kombe kwa kuwa halmashauri inayoongeza kiwango cha Ufaulu Kidato cha nne kwa miaka mitatu mfululizo kuanzia 2019 - 2021 huku shule ya Sekondari Ilboru ikiongoza kwa shule za serikali.
Jumla ya wanafunzi 13 wa shule ya sekondari Ilboru wamefanikiwa kupata zawadi za kuongoza kitaifa pamoja na kuongoza kimasomo.
Hata hivyo shule ya Sekondari Mwandeti ni miongoni mwa shule iliyokuwa kwenye shule 10 bora kwa miaka mitatu, ikishika nafasi ya 6, 7 na ya 8, Shule ya sekondari Mringa ikiwa na wanafunzi waliongoza kwenye masomo ya Biashara 'ECA'.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.