Na. Elinipa Lupembe.
Serikali kupitia mradi wake wa Lipa kutokakana na Matokeo, P4R imetoa kiasi cha shilingi milioni 750, kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika sekta ya elimu na afya, hàlmashauri ya Arusha, ikiwa ni utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwenye bajeti ya mwaka wa fedha 2020/2021.
Akizungumza na wmandishi wetu ofisini kwake, Mkurugenzi mtendaji halmashauri ya Arusha, Saad Mtambule, amethibitisha kupokea kiasi hicho cha fedha na kufafanua kuwa, serikali imeelekeza fedha hizo kutekeleza miradi ya ujenzi wa miundombinu ya shule ikiwa ni vyumba vya 14 vya madarasa, matundu 12 ya vyoo, pamoja na mabweni manne katika shule mbili za sekondari.
Aidha Mkurugenzi huyo, amefafanua kuwa, upatikanaji wa fedha hizo umekuja baada ya halmsahuri hiyo kutekeleza mirada ya EP4R kwa ufanisi mkubwa, na kuahidi kuendelea kusimamia matumizi ya fedha hizo kwa kuzingatia kanuni, sheria, taratibu na miongozo ya matumizi ya fedha za serikali, huku miradi hiyo ikitekelezwa kwa ubora na kukamilika kwa wakati.
"Tumepata fedha hizi, kutokana na halmashauri yetu, kutekeleza kwa ustadi miradi iliyotangulia ya P4R, tulihakikisha miradi tuliyoletewa na serikali ilitekelezwa kwa kuzingatia kanuni, sheria, taratibu na miongozo ya matumizi ya fedha za umma, na tutahahakishisha fedha hizi zitatekeleza miradi hiyo kama iliyoelekezwa kwa manufaa watanzania" ameweka wazi Mkurugenzi huyo.
Naye Afisa Mipango halmashauri ya Arusha, Anna Urio ameweka wazi kuwa, kiasi hicho cha shilingi milioni 750, zitatumika kujenga vyumba 14 vya madarasa na miundombinu ya vyoo kwa gharama ya shilingi milioni 280, shilingi milioni 320 kujenga mabweni manne ya shule mbili za sekondari, huku shilingi milioni 150 zikielekezwa katika ukamilishaji wa zahanati tatu.
"Shilingi milioni 280, zitajenga vyumba 14 vya madarasa katika shule tatu za msingi, na shule 4 za sekondari kwa gharama ya shilingi milioni 40 kwa darasa, na shilingi milioni 150, zitakwenda kukamilisha ujenzi wa zahanati 3 kwa gaharama ya shilingi milioni 50 kila zahanati na ujenzi wa mabweni manne kwa shule mbili za sekondari kwa shilingi milioni 320, milioni 160 kwa kila shule" amefafanua Afisa Mipango huyo.
Hata hivyo Afisa Mipango huyo, amesisistiza kuwa fedha hizo zitatumia utaratibu wa 'forced account' kwa kutumia 'Local fundis' pamaja na matumzi ya rasilimali zinazopatikana katika maeneo husika, huku kukiwa na ushirikishwaji wa wananchi kupitia kamati za ujenzi pamaja na viongozi wa ngazi za vijiji na kata husika.
Awali imeelezwa kuwa, miradi hiyo itatkelezwa katika shule za msingi Kambi ya Maziwa, Ilboru na Olimringaringa, shule za sekondari Kiranyi, Kiseriani, Likamba, Einoti na Iking'a zote zikitekeleza ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa kwa kila shule pamoja na samani, ujenzi wa mabweni manne kwa shule mbili za sekondari pamoja na ukamilishaji wa ujenzi wa zahanati za Ilkurot, Laroi na Kigongoni, zote zikiwa kwenye kata za pembezoni.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.