Na. Elinipa Lupembe.
Kufuatia utekelezaji wa mapango wa bajeti ya mapato na matumizi iliyopitisha na kuidhinishwa na Bunge la Jamhuri wa Muungano wa Tanzania kwa mwaka wa fedha 2019/2020, halmashauri ya Arusha, ilifanikiwa kutekeleza bajeti hiyo kwa zaidi ya asilimia 80.
Akizungumza wakati wa mkutano wa Baraza la Madiwani la mapitio ya utekelezaji wa mpango wa mapato na matumizi ya bajeti kwa mwaka wa fedha unaoendelea wa 2020/2021, Afisa Mipango halmashauri ya Arusha, Anna Urio, ameeleza kuwa, kwa mwaka wa fedha 2019/2020, halmashauri ilifanikiwa kutekeleza mpango wa bajeti ya mapato na matumizi kwa asilimia 80.6 kama ilivyoidhinishwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Afisa Mipango Anna, amesema kuwa kwa mwaka wa fedha 2020/2021, halmashauri ya Arusha, imefanikiwa kutekeleza bajeti kwa kiasi cha shilingi bilioni 42.5 sawa na asilimia 80.6 kutoka kiasi cha shilingi bilioni 52.8 iliyoidhinishwa na Bunge la Bajeti mwaka 2020.Amefafanua kuwa katika utekelezaji wa mpango huo wa bajeti, halmashauri imetekeleza bajeti ya shilingi bilioni 3.4 kwa ajili ya Ruzuku ya miradi ya maendeleo kwa asilimia 63.04, fidia ya mapato shilingi milioni 11 sawa na asilimia 91.71, Ruzuku ya Mishahara shilingi bilioni 33.7 sawa na asilimia 83.1, Ruzuku ya matumizi mengine shilingi bilioni 1.4 sawa na asilimia 85.18 pamoja na mapato ya ndani kiasi cha shilingi bilion 5.0 sawa na asilimia 10.Hata hivyo, serikali imefanikiwa kutumia fedha kupitia miradi ya maendeleo kiasi cha shilingi bilioni 3.4 kwa zaidi ya asilimia 64.64 kutoka shilingi bilioni 5.37 zilizoidhinishwa, huku halmashauri ikitumia kiasi cha shilingi milioni 317.9 sawa na asilimia 29 kutoka shilingi bilioni 5.37 zilizoidhinishwa.
Aidha katika kutekeleza miradi ya Lipa kutokana na Matokeo - Education paymente for result - EP4R kwa shule za msingi, serikali imetekeleza miradi ya ujenzi ya miundombinu ya vyumba 15 vya madarasa na matundu 18 ya vyoo kwa shule za msingi 7, kwa gharama ya shilingi milioni 319.8 sawa na asilimia 100, kwa upande wa Elimu sekondari, halmashauri imetekeleza miradi ya Lipa kutokana na Matokeo - EP4R, kwa kutekeleza ujenzi wa vyumba 7 vya madarasa, bweni 1, nyumba mbili za walimu zenye sehemu 2 (2 in 1) kwa gharama ya shilingi milioni 331.0 sawa na asilimia 100.
Halmashauri pia imefanikiwa kupokea fedha kutoka serikali kuu, na kutekeleza miradi ya ujenzi wa vyumba 4 vya madarasa ya shule ya sekondari Sokoni II kwa gharama ya shilingi milioni 280 na ujenzi na ukamilishaji wa Zahanati ya Musa kwa gharama ya shilingi milioni 200, pamoja na kiasi cha shilingi milioni 80 kwa ajili ya ujenzi wa bweni shule ya sekondari ya Einoti, fedha kutoka Mamlaka ya Elimu Tanzania - TEA.
Hata hivyo halmashauri imefanikiwa kutekeleza agizo la serikali la uwezeshaji wananchi kiuchumi kwa kutoa mikopo siyo na riba kwa vikundi vya wajasiriamali wanawake, vijana na walemavu, kwa kutoa asilimia 10 ya mapato yake ya ndani, kiasi cha shilingi milioni 184.4 sawa na asilimia 100 kutoka shilingi milioni 311.3 zilizokisiwa kutumika huku kiasi cha shilingi milioni 76.5 zikikopeshwa kupitia fedha za marejesho ya wajasiriamali.
Aidha, jumla ya vikundi 66 vya wajasiriamali, vilifanikiwa kupatiwa mikopo ya bila riba, huku vikundi 56 vya wnakawake vikikopeshwa kiasi cha shilingi milioni 212 na vikundi 10 vya vijana vyenye vijana walikopeshwa kiasi vah shilingi milioni 49.
Awali, mkutano huo wa Baraza la Madiwani wa kufanya tathmini ya mapitio ya mpango wa mapato na matumizi ya bajeti kwa mwaka wa fedha uliopita 2019/2020, ikiwa ni mchakato wa maandalizi wa rasimu ya mpango wa bajeti wa mapato na matumizi ya halmashauri kwa mwaka ujao wa fedha 2021/2022, mkutano uliofanyika kwenye Ukumbi wa mikutano wa halmashauri hiyo, kwa mujibu wa sheria, kanuni na taratibu za uendeshaji wa serikali za mitaa, mchakato ambao unatoa mwanga wa mpango wa bajeti wa mwaka ujao wa fedha wa 2021/2022.
Afisa Mipango, Halmashauri ya Arusha, Anna Urio , akiwasilisha taaarifa ya tathmini ya utekelezazaji wa Mpango Bajeti ya Mapato na Matumizi, iliyotekelezwa kwa mwaka wa fedha 2019/2020, wakati wa mkutano wa Baraza la Madiwani.
Mkurugenzi Mtendaji, Halmashauri ya Arusha, Saad Mtambule , akitolea ufafanuzo hoja za wajumbe zilizzojitokeza, wakati wa mkutano wa Baraza la Madiwani, la kujadili tathmini ya utekelezazaji wa Mpango Bajeti ya Mapato na Matumizi, iliyotekelezwa kwa mwaka wa fedha 2019/2020
Waheshimiwa Madiwani, wakifuatia uwasilishwaji wa tathmini ya utekelezazaji wa Mpango Bajeti ya Mapato na Matumizi, iliyotekelezwa kwa mwaka wa fedha 2019/2020.
Mbunhe wa Jimbo la Arumeru Magharibi, Mheshimiwa Noah Lembris, akizungumza wakati wa mkutano wa Baraza la Madiwani, la kujadili tathmini ya utekelezazaji wa Mpango Bajeti ya Mapato na Matumizi, iliyotekelezwa kwa mwaka wa fedha 2019/2020
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.