• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe |
Arusha District Council
Arusha District Council

Serikali ya jamuhuri ya Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili Makuu
    • Mikkati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara na Vitengo
      • Utawala na Utumishi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Fadha na Biashara
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliji
      • Ardhi na Maliasili
      • Maji
      • Works
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo na Umwagiliaji na Ushirika
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Internal Audit
      • Nyuki
      • Uchaguzi
      • UKIMWI/ AIDS
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Livestock
    • Wadau wa Maendeleo
  • Huduma Zetu
    • Health
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Utawala Fedha na Mipango
      • Elimu Afya na Maji
      • Kudhibiti UKIMWI
      • Maadili ya Madiwani
      • Uchumi Ujenzi na Mazingira
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Vikao vya Timu ya Uendeshji ya Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mktaba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa UMMA
    • Video za Shoghuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

ARUSHA DC YATOA MILIONI 384 MKOPO KWA VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU

Posted on: November 1st, 2021

Na. Elinipa Lupembe

Halmashauri ya Arusha imetoa fedha, kiasi cha shilingi miloni 384 kwa vikundi 50 vya Wanawake, na Vijana, pamoja na watu wawili wenye Ulemavu, ikiwa ni utekelezaji wa maagizo ya Serikali kwa halmashauri kutoa asilimia 10 ya mapato yake ya ndani kwa makundi hayo matatu, mikopo isiyo na riba, ikiwa ni utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi.

Akizungumza wakati wa hafla fupi ya kutoa mikopo hiyo iliyofanyika kwenye viwanja vya halmashauri hiyo, Mkuu  wa Wilaya ya Aruemru, Mhandisi Richard Ruyango, ameupongeza uongozi wa halmashauri ya Arusha, kwa kutekeleza kwa vitendo, azimio hilo la Serikali na kuwataka wanavikundi hao kuhakikisha wanatumia fedha hizo kwa malengo waliyokusudia na si vinginevyo.

Amesema kuwa, mikopo ya asilimia 10 ya mapato ya ndani inatokana na kodi zenu zinazokusanywa na halmashauri yenu kupitia vyanzo mbalimbali vya mapato, hivyo serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na mjeshimiwa Rais, mama Samia Suluhu Hassan, ikaona ni vema kurudisha asilimia 10 ya mapato yake kwa wananchi kwa kuwapa mikopo isiyokuwa na riba, ili wananchi waweze kunufaika kwa kujipatia mitaji itakayozalisha faida kwa kuongeza kipato cha familia na taifa kwa ujumla.

Hata hivyo ameshangazwa na idadi ndogo ya vikundi vya vijana ukilinganisha na vikundi 40 vya wanawake vilivyojitokeza kuomba mikopo hiyo, kwa vijana kushindwa kujitokeza kutumia fursa hiyo adhimu inayotolewa na serikali yao, jambo ambalo linaendelea kuzorotesha maendeleo ya vijana nchini, vijana mbao taifa linawategemea.

"Ninawashangaa sana vijana, katika shilingi milioni 384, vikundi vya vijana wanapata milioni 85 tuu, niwasihi vijana wangu, tambueni serikali yenu inawajali, tumieni fursa hii kwa kuchukua hatua ya kujiunga kwenye vikundi ili kupata mikopo hii, anzisheni biashara ndogo ndogo kupitia raslimali zinazopatikana katika maeneo yenu, msiogope kuthubutu vijana wangu" amesistiza Mkuu huyo wa Wilaya.

Aidha ameiagiza Idara ya Maendeleo ya Jamii, kuendelea kutoa elimu kwa vijana kwa kuwafikia vijana wengi zaidi katika maeneo yao, ili wapate uelewa juu ya mikopo hii na kujiunga kwenye vikundi vitakavyowawezesha kutumia fursa hii ya kupata mikopo isiyo na riba inayotolewa na serikali yao.

Naye Mwenyekiti wa Halmashauri ya Arusha, Mheshimiwa Ojung'u Salekwa, amewasihi wanavikundi hao hasa kina mama, kuwa makini na miezi hii ya sherehe kwa kuacha kushawishika kutumia fedha hizo kwenye sherehe zinazofanyika kila mwisho wa mwaka.

"Mmepokea fedha hizi, kipindi ambacho kuna sherehe nyingi za kufunga mwaka, msije mkatumia fedha hizo kwenye ubarikio, 'mbesii' za kina mama, wala kununua vitenge vya 'wax' doti 60 kwa ajili ya 'send off', tumieni fedha hizo kuzalisha na kujionhezea kipato cha familia pamoja na kurejesha kwa wakati" amesisitiza Mwenyekiti huyu wa Halmashauri.

Mkurugenzi Mtendaji halmashauri ya  Arusha, Seleman Msumi, licha ya kuwasisitiza wanavikundi hao, kuwa fedha hizo ni za mkopo na si zawadi, amefafanua kuwa katika mapato ya halmashauri kwa kipindi cha miezi mitatu ya robo ya kwanza ya mwaka wa fedha 2021/2022, halmashauri imetenga jumla ya shilingi milioni 384 ikiwa ni asilimia 10 ya fedha zilizokusanywa, kwa ajili ya kutoa mikopo isiyokuwa na riba kwa vikundi vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu.

Amebainisha kuwa kiasi hicho cha fedha kimetolewa kwa vikundi 40 vya wanawake waliokopeshwa shilingi milioni 295, vikundi 10 vya vijana waliokopeshwa shilingi milioni 86, na watu wawili wenye ulemavu waliokopeshwa shilingi milioni 4 na kufanya jumla ya shilingi milioni 384.

Hata hivyo wanavikundi hao wameishukuru serikali ya awamu ya sita, kwa kuwajali wananchi wa hali ya chini kwa kuwapa mikopo isiyokuwa na riba huku wakiahidi kwenda kutumia fedha hizo kufanya biashara walizokusudia kwa kuzalisha faida pamoja na kurejesha kwa wakati.

Elibariki Munga aliyepokea mkopo huo kupitia kundi la watu mwenye ulemavu, amethibitisha kuwa mwaminifu katika kurejesha fedha hizo huku akisistiza kurejesha kwa uaminifu fedha alizopokea, kutokana na ukweli kwamba serikali kwa sasa imewathamini sana watu wenye ulemavu tofauti na hapo awali.

"Tutakuwa waminifu katiaka kurejesha mikopo hii, ninaamini kati ya watu ambao watakuwa waaminifu kurejesha fedha hizo ni sisi watu wenye ulema, niaahidi kurejsha fedha hizi kwa wakati bila usumbufu wowote" amethibitisha Munga.


PICHA ZA MATUKIO.

Mkuu wa wilaya ya Arumeru, Mhandisi Richard Ruyango akizungumza na wanavikundi vya Wanawake, Vijana na watu wenye Ulemavu, wakati wa hafla fupi ya kuwakabidhi mikopo ya asilimia 10 ya mapato ya ndani ya halmashauri ya Arusha kwa mwaka kipindi cha robo ya kwanza kwa mwaka wa fedha 2021/2022.




Mwenyekiti wa halmashauri ya Arusha, Mheshimiwa Ojung'u Salekwa akiwaasa wanavikundi vya Wanawake, Vijana na watu wenye Ulemavu, wakati wa hafla fupi ya kuwakabidhi mikopo ya asilimia 10 ya mapato ya ndani ya halmashauri ya Arusha kwa mwaka kipindi cha robo ya kwanza kwa mwaka wa fedha 2021/2022.


Baadhi ya wanavikundi vya Wanawake, Vijana na watu wenye Ulemavu, wakifuatilia mawasilisho mbalimbali kutoka kwa viongozi na watalamu, wakati wa hafla fupi ya kuwakabidhi mikopo ya asilimia 10 ya mapato ya ndani ya halmashauri ya Arusha kwa mwaka kipindi cha robo ya kwanza kwa mwaka wa fedha 2021/2022.



Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA MKATABA ENABOISHU FM - ARUSHA DC May 26, 2025
  • ORODHA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO 2023 ARUSHA DC June 11, 2023
  • ZIARA YA WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS TAMISEMI, MHE. MOHAMED O. MCHENGERWA 17 SEPTEMBA 2024 September 13, 2024
  • MTIHANI WA DARASA LA SABA 11-12/09/2024 September 09, 2024
  • Tazama zote

Habari mpya

  • VIONGOZI WA DINI WAPEWA ELIMU YA CHAKULA BORA

    May 28, 2025
  • VIONGOZI WA DINI WAPEWA ELIMU YA AFYA YA MAMA NA MTOTO

    May 27, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA MKATABA

    May 26, 2025
  • RC MAKONDA ATEMBELEA NA KUKAGUA MRADI WA UJENZI WA MAHAKAMA YA AFRIKA ARUSHA

    May 25, 2025
  • Tazama zote

Video

Video zaidi

Viunganishi vinavyoingiliana

  • Leseni ya vileo
  • Fomu ya ukaguzi

Viunganishi vinavyohusiana

  • Tovuti kuu ya serikali
  • Tamisemi
  • Utumishi portal
  • Wakala wa serikali mtandao
  • Mkoa wa arusha
  • ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Sekei Road

    Anuani ya posta: 2330 Arusha

    Simu : +255 027 2502737

    Simu: 073 65000476

    Barua pepe: ded@arushadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.