Na Elinipa Lupembe
Halmashauri ya Arusha imefanikiwa kutwaa jumla ya makombe 8 kwenye mashindano ya UMITASHUMTA ngazi ya mkoa, mashindano yaliyomalizika mwishoni mwa wiki iliyopita.
Halmashauri ya Arusha, imefanikiwa kutwaa ubingwa ngazi ya Mkoa kwa kuwa washindi wa kwanza soka la wavulana, nafasi ya pili soka wasichana, netibol wasichana, mpira wa wavu, mshindi wa tatu goalball wasichana, mshindi wa pili goalbal wavulana pamoja fani za ndani ngoma na kwaya.
Hata hivyo katika mashindano hayo ngazi ya mkoa, jumla ya wanamichezo 47 kutoka shule za halmashauri ya Arusha wamechaguliwa kati ya wanamichezo 120 watakaowakilisha timu ya Mkoa wa Arusha kwenye mashindano ya UMITASHUMTA ngazi ya Taifa yatakayofanyika mkoani Tabora.
ARUSHA DC USHINDI NI JADI YETU.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.