ARUSHA NA URUSI ZAKUBALIANA KUSHIRIKIANA KWENYE SEKTA MBALIMBALI IKIWEMO YA UTALII.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul Christian Makonda amekutana na kuzungumza na Balozi wa Urusi nchini Tanzania Mhe. Andrey Avetisyan na kukubaliana kuendelea kushirikiana katika kukuza Utalii wa Arusha na kuvutia wawekezaji wengi zaidi raia wa Urusi kuja kuwekeza Mkoani Arusha.
Kwenye mazungumzo yao, Mhe. Makonda amwambia Balozi huyo wa Urusi kuwa Mko wa Arusha una fursa mbalimbali za uwekezaji zikiwemo Hoteli za Kitalii zenye hadhi ya nyota 5, Kumbi za Mikutano za Kimataifa, pia sekta ya Kilimo cha maua na mbogamboga pamoja na uwekezaji kwenye sekta ya usafiri wa Anga kutokana na mahitaji makubwa ya Utalii kwani Arusha ndiyo lanho kuu la Utalii Nchini.
Balozi Avetisyan kando ya Ratiba zake nyingine, Leo alhamisi Oktoba 17, 2024 anakutana na wafanyabiashara na Wawekezaji wa Kirusi waliopo Mkoani Arusha ambapo pia Mhe. Makonda ameahidi kushirikiana na Wawekezaji hao katika kurahisisha mazingira ya uwekezaji Mkoani hapa na kusema kuwa Ofisi yake ipo wazi muda wote katika kuhudumia wageni na wenyeji wa Mkoa huo ulio muhimu kwa Utalii, biashara na shughuli mbalimbali za kidiplomasia.
Ikumbukwe kuwa mwanzoni mwa miaka ya 1960 mpaka 1980 Nchi ya Urusi (USSR) chini ya sera zake za Kijamaa ilisaidia ukombozi wa Nchi nyingi za Afrika ilishirikiana bega kwa bega kutoa misaada wa hali na mali ikiwemo mafunzo na rasimali nyingine ili kuondoa utawala wa kikoloni na kuziwezesha Nchi za Afrika kuwa huru na kujitawala.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.