Na Elinipa Lupembe.
ASAS ya Kiraia ya AAIDRO ya kanisa Katoliki Jimbo Kuu Arusha chini ya Idara ya Jinsia na Wanawake imezindua mradi wa kuwainua wananchi wenye hali ya chini kiuchumu katika kata za Nduruma na Bwawani Halmashauri ya Arusha.
Akizungumza wakati wa kuutambulisha mradi huo, kwenye ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji halmashauri ya Arusha, kwa niaba ya Kanisa Katoliki Padri Faustine Moshi, amesema kuwa mradi huo utatekelezwa kwa kipindi cha mwaka mmoja na utahusisha makundi rika tofauti kwa lengo la kuwawezesha wananchi kijiinua kiuchumi na kijamii.
Aidha Padri Mosha amesema kuwa Kanisa limeona ni vema kushirikiana na Serikali kuwahudumia wananchi katika sekta nyingine zaidi ya ile ya kiroho, na kuongeza kuwa wanatarajia kupata ushirikiano mkubwa kutoka kwa watalamu wa halmashauri ili kufikia lengo la kanisa na malengo ya serikali ya kuwahudumia wananchi.
“Utekelezaji wa mradi huu utagharimu takribani shilingi milioni 230 na kuwajengea uwezo watu 200 kupitia vikundi, hivyo ni matumaini yetu, kazi hii itafanywa na kanisa na watalamu kutoka serikalini kupiti halmashauri, kwa pamoja tutafikia lengo”.Amesisitiza Padri Mosha.
Hata hivyo Mkurugenzi Mtendaji halmashauri ya Arusha Seleman Msumi, amelishukuru Kanisa kupitia ASAS ya AAIDRO kwa kuona umuhimu wa kuunga mkono juhudi za serikali za kuwajengea uwezo wananchi kujikwamua kiuchumi, kazi ambayo ingefanywa na serikali.
“Kama Hamashauri tuko tayari kushirikiana na kanisa kwa kuzingatia jukumu la serikali ni kuweka mazingira rafiki kwa mashirika yanayofanya kazi za kuhudumia jamii kulingana na mpango mkakati wa serikali, tunao watalamu wa kutosha katika idara zote, hivyo watashirikiana nanyi katika hatua zote za utekelezaji wa mradi huu”. Amesbainisha Mkurugenzi Msumi.
Aidha amelitaka shirika hilo Kwenda kutekeleza mradi huo kulinga na andiko la mradi na si vinginevyo, sambamba na kuwasilisha taarifa ya utekelezaji wa mradi huo kila robo ya mwaka kwenye vikao vya kisheria vya mashirika yasiyo ya kiserikali.
Naye mratibu wa mradi huo, Irene Moshi, amefananua kuwa mradi huo utajikita katika kuwapa mafunzo wakulima na kufanya kilimo cha kisasa, kilimo biashara kulingana na Ajenda 10/30, kuwajengea uwezo wajasiriamali pamoja na masuala mtambuka ya kupinga ukatili wa kijinsia kwa wanaume, wanawake na watoto ikiwemo ukeketaji na ndoa za utotoni.
“Kupitia mradi huu tunategemea kuwaiwezesha jamii kuwa na uwezo wa kujikomboa kifkra, uwezo wa kujitegemea kiuchumi katika kujipatia pato la familia, pamoja na kuwa na jamii huru isiyokuwa na ukatili wa aina yoyote katika masuala ya kijinsia”. Amesistiza Irene
Awali kwa sasa mradi huo uko katika hatua za awali, utatekelezwa kwa muda wa mwaka mmoja na unategemea kukamilika ifikapo Juni 2023.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.