• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe |
Arusha District Council
Arusha District Council

Serikali ya jamuhuri ya Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili Makuu
    • Mikkati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara na Vitengo
      • Utawala na Utumishi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Fadha na Biashara
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliji
      • Ardhi na Maliasili
      • Maji
      • Works
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo na Umwagiliaji na Ushirika
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Internal Audit
      • Nyuki
      • Uchaguzi
      • UKIMWI/ AIDS
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Livestock
    • Wadau wa Maendeleo
  • Huduma Zetu
    • Health
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Utawala Fedha na Mipango
      • Elimu Afya na Maji
      • Kudhibiti UKIMWI
      • Maadili ya Madiwani
      • Uchumi Ujenzi na Mazingira
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Vikao vya Timu ya Uendeshji ya Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mktaba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa UMMA
    • Video za Shoghuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

ASAS YA ZOE AFRICA (TZ) YAWAKWAMUA KIUCHUMI VIJANA YATIMA NA WAISHIO KWENYE MAZINGIRA MAGUMU

Posted on: December 3rd, 2022

Na Elinipa Lupembe

ASAS ya kiraia ya ZOE AFRICA (TZ) imefanikiwa kuwaainua kiuchumi na kijamii vijana yatima na wale wanaoishi kwenye mazingira hatarishi, kwa kuwajengea uwezo kulingana na matakwa na matamanio yao pamoja na kuwapa mitaji na vifaa vya ofisi.

ASAS hiyo imefikia hatua hiyo kutokana na changamoto zinazolikabili kundi hilo la vijana wa wenye umri wa miaka 15 - 20, za kukatisha ndoto zao kutokana na kuondokewa na wazazi/mzazi na wenginee kutokana na hali duni za maisha ya familia zao.

Akizungumza wakati wa mahafali ya kuhitimu vijana 156, Mkuu wa wilaya ya Arusha, Mhe. Saidi Mtanda amempongeza mkurugenzi wa ZOE kwa kazi kubwa inayofanywa na shirika hilo, ya kurejesha matumaini ya vijana ambayo yalipotea na pengine kutoweka kabisa.

Mkuu huyo wa Wilaya ameweka wazi kuwa, Serikali inatambua na kuthamini kazi inayofanywa na mashirika yasiyo ya kiserikali, shirika linafanya kazi ambayo ingepaswa kufanywa na serikali, amewapongeza kwa kuunga mkono juhudi za serikali na kuahidi kushirikiana nao.

Ameongeza kuwa, kazi hii si kwa mujibu wa serikali  pekee bali ni kazi ya Mungu, mnafanya kazi ya kuwaokoa vijana waliokata tamaa kutoka kwenye wimbi la kihalifu, uzururaji na uvutaji bangi na kuwa vijana wenye heshima kwa jamii na Taifa, malipo yake mtayapata kwa Mungu na si hapa duniani.

"Kundi hili la vijana 156, bila ZOE lingekuwa kwenye hali gani kimaisha, mmetuondolea vijana wasiokuwa na mwelekeo na kuwaleta kwenye kundi la vijana, watakaokwenda kulijenga Taifa la Tanzania, ". Amesisitiza Mhe. Mtanda

Akiwasilisha taarifa ya shirika hilo, Mkurugenzi wa ZOE AFRICA (TZ), Mchungaji Trice Shumbusho, amesema kuwa, katika maafali hayo, jumala ya vijana 150,wamehitimu baada ya kupata mafunzo kwa muda wa miaka mitatu na kufanikiwa kuwapa ujuzi na maarifa, ambao tayari wameshaweza kujitegemea kwa kuanzisha biashara.

"Wahitimu wa leo, wamejengewa uwezo na tayari wameweza kuanzisha biashara kwa kufungua ofisi zao, huku ZOE ikiwapatia vifaa vya ofisi pamoja na pesa ya kodi ya miezi mitatu ya awali, lakini shirika litaendelea kuwasimamia kwa muda mpaka hapo tutakapoona biashara zao zimesimama vizuru".Amefafanua Mkurugenzi huyo

Hata hivyo wahitimu hao, licha ya kulishukuru shirika hilo kwa kuwaleta pamoja, kuwatunza, kuwapa ujuzi na maarifa pamoja na kuwapatia vifaa vya ofisi, jambo ambalo wamekiri ni neema ya Mungu kwa ZOE kuwafanyia huduma hiyo yenye thamani katika maisha yao na familia zao.

Edna Lesikari mkazi wa Mlangarini, amekiri kuwa awali alikuwa na ujuzi mdogo sana wa kushona, lakini ZOE wamempa mafunzo ya ushonaji pamoja na mashine ya cherehani ambapo tayari anamiliki ofisi yake na sasa anauwezo wa kushoma hadi nguo za kiume.

"Nilikuwa na fani ya ususi, lakini sikuwa na mtaji wala vifaa, ZOE wameniwezesha kujifunza fani hiyo kwa ngazi ya juu na kunipa vifaa vilivyoniwezesha kufungua saloni yangu, wakanipa mtaji, ambapo sasa ninauwezo wa kujitegemea, kujikumu kimaisha na kuwahudumia ndugu zangu" . Amesema mwanafunzi Rehema Lucas

Naye Veronica Samson amebainisha kuwa hapo awali hakuwa na uhakika na maisha yake, aliishi kwa kufanya vibarua kwa mama lishe, ZOE imemuwezesha kujifunza kutengeneza 'Peanut butter' na kumpa mtaji, unaomuwezesha kuendesha biashara yake, biashara ambayo inamfanya kujiamini,kujithamini na kujiona anao uwezo wa kuishi kwa malengo.

Shirika la ZOE AFRICA (TZ) linafanya kazi mkoani Arusha kwenye halmashauri za Arusha na Jiji la Arusha, lilianza rasmi mwaka 2019 likiwa na vikundi 10 na vijana 256 wakiwa na wategemezi takribani 737 mpaka sasa kuna vikundi 40 vyenye vijana 968 na wategemezi 3wateg


ARUSHA 

KaziInaendelea ✍✍✍





Matangazo

  • TANGAZO LA KAZI ZA MKATABA HALMASHAURI YA WILAYA YA ARUSHA August 14, 2025
  • ORODHA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO 2023 ARUSHA DC June 11, 2023
  • ZIARA YA WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS TAMISEMI, MHE. MOHAMED O. MCHENGERWA 17 SEPTEMBA 2024 September 13, 2024
  • MTIHANI WA DARASA LA SABA 11-12/09/2024 September 09, 2024
  • Tazama zote

Habari mpya

  • KUFUATILIA NA USAMIZI WA HAKI ZA MTOTO KATIKA JAMII NI JAMBO MUHIMU

    August 25, 2025
  • RAIS SAMIA AMUAPISHA AMOS MAKALLA KUWA MKUU WA MKOA WA ARUSHA

    August 26, 2025
  • DKT. JAHANNES LEMBULUNG' LUKUMAY ACHUKUWA FOMU YA UGOMBEA UBUNGE WA CCM JIMBO LA ARUMERU MAGHARIBI

    August 25, 2025
  • KIKAO KAZI CHA WENYEVYITI WA BODI NA WATENDAJI WAKUU WA TAASISI ZA UMMA (CEOs Forum 2025)

    August 24, 2025
  • Tazama zote

Video

Video zaidi

Viunganishi vinavyoingiliana

  • Leseni ya vileo
  • Fomu ya ukaguzi

Viunganishi vinavyohusiana

  • Tovuti kuu ya serikali
  • Tamisemi
  • Utumishi portal
  • Wakala wa serikali mtandao
  • Mkoa wa arusha
  • ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Sekei Road

    Anuani ya posta: 2330 Arusha

    Simu : +255 027 2502737

    Simu: 073 65000476

    Barua pepe: ded@arushadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.