• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe |
Arusha District Council
Arusha District Council

Serikali ya jamuhuri ya Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili Makuu
    • Mikkati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara na Vitengo
      • Utawala na Utumishi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Fadha na Biashara
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliji
      • Ardhi na Maliasili
      • Maji
      • Works
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo na Umwagiliaji na Ushirika
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Internal Audit
      • Nyuki
      • Uchaguzi
      • UKIMWI/ AIDS
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Livestock
    • Wadau wa Maendeleo
  • Huduma Zetu
    • Health
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Utawala Fedha na Mipango
      • Elimu Afya na Maji
      • Kudhibiti UKIMWI
      • Maadili ya Madiwani
      • Uchumi Ujenzi na Mazingira
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Vikao vya Timu ya Uendeshji ya Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mktaba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa UMMA
    • Video za Shoghuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

ASILIMIA 88 YA WANAFUNZI WALIOPANGIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA 2021 ARUSHA DC,  WAANZA RASMI MASOMO YAO SEKONDARI

Posted on: February 24th, 2021

.Na. Elinipa Lupembe.

Jumla ya Wanafunzi 7,018 waliochaguliwa kujiunga na Kidato cha kwanza mwaka 2021 halmashauri ya Arusha tayari wameanza mosomo rasmi, katika shule sekondari za serikali walizopangia, kufuatia kufaulu mtihani wa darasa la saba uliofanyika mwishoni mwa mwaka 2020.

Afisa Elimu sekondari, halmashauri ya Arusha, Mwl. Menard Lupenza, ameleza kuwa, jumla ya wanafunzi 7, 018 sawa na asilimi 88, waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza na kupangiwa kwenye shule za sekondari za serikali za halmashauri ya Arusha, tayari wameripoti shuleni na kuanza rasmi safari yao ya masomo ya elimu ya sekondari. 

Afisa Elimu Lupenza amefafanua kuwa kati ya wanafunzi 7,886 waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza mwaka wa masomo 2021, wanafunzi 7, 018 tayari wamekwisharipotii kwenye shule walizopangiwa na kuanza masomo yao ya sekondari ambapo kati ya hao 7,018 wasichana ni 3,153 na wavulana 2,746,  na kuongeza kuwa kati ya hao, wanafunzi 607 wamehamia kwenye shule nyingine za serikali ndani na nje ya halmashauri ya Arusha.

"Kati ya wanafunzi 7,018, tumefuatilia  na kugundua kuwa wanafunzi 512 wamekwenda kujiunga na shule za binafsi, na tumejiridhisha na uandikishwaji wa wanafunzi hao kwenye shule hizo za binafsi, lakini jumla ya wanafunzi 868, wasichana 432  na wavulana 436 sawa na asilimia 1, hawa bado hawajaripoti kwenye shule walizopangiwa, licha ya kuwa muda wa kujisajili unaendelea, jitihada za kuwatafuta wanafunzi hao zinaendelea kwa kushirikiana na maafisa watendaji wa kata na vijiiji na viongozi serikali za wa vijiji pamoja na wazazi na walezi wa watoto hao". Amefafanua Afisa Elimu huyo.

Naye mkuu wa shule ya sekondari Oldonyowas, mwalimu Richard Mugabuso amethibitisha kupokea jumla ya wanafunzi 67 kati ya wanafunzi 83 waliopangiwa, na kuongeza kuwa, jumla ya wanafunzi 63 walihamia shuleni hapo kutoka shule nyingine walizopangiwa na wanafunzi 12 wamehama kwenda shule nyingine za sekondari, huku wanafunzi 4 tu hawajaripoti shuleni hapo mpaka sasa.

Hata hivyo mkuu wa shule ya sekondari Mukulat, mwalimu Meiseyeki Saiboku, naye amethibitisha kupokea jumla ya wanafunzi 279 wavulana 117 na wasichana 163 kati ya wanafunzi 300, waliopangiwa shuleni hapo kuanza masomo ya sekondari Januari mwaka 2021.

Wakati huo huo, jitihada za ukamilishaji mradi wa ujenzi wa vyumba 52 vya madarasa, unaendelea vema lengo likiwa ni maandalizi ya kupokea wanafunzi wa kidato cha kwanza mwaka ujao 2022, kati ya vymba hivyo 52, vyumba 42 viko hatua za ukamilishaji, vyumba 5 viko kwenye hatua ya lenta, vyumba 4 viko kwenye kupandisha kuta na chumba 1 kiko kwenye hatua ya msingi.

Awali uongozi wa halmashauri ya Arusha, unawataka wazazi na walezi ambao hawajawawezesha watoto wao waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza mwaka 2021, kuhakikisha wanafunzi hao wanarepoti kwenye shule walizopangiwa, na kushindwa kufanya hivyo, seriakli itawachukulia hatua za kisheria.






Matangazo

  • TANGAZO LA KAZI ZA MKATABA HALMASHAURI YA WILAYA YA ARUSHA August 14, 2025
  • ORODHA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO 2023 ARUSHA DC June 11, 2023
  • ZIARA YA WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS TAMISEMI, MHE. MOHAMED O. MCHENGERWA 17 SEPTEMBA 2024 September 13, 2024
  • MTIHANI WA DARASA LA SABA 11-12/09/2024 September 09, 2024
  • Tazama zote

Habari mpya

  • KUFUATILIA NA USAMIZI WA HAKI ZA MTOTO KATIKA JAMII NI JAMBO MUHIMU

    August 25, 2025
  • RAIS SAMIA AMUAPISHA AMOS MAKALLA KUWA MKUU WA MKOA WA ARUSHA

    August 26, 2025
  • DKT. JAHANNES LEMBULUNG' LUKUMAY ACHUKUWA FOMU YA UGOMBEA UBUNGE WA CCM JIMBO LA ARUMERU MAGHARIBI

    August 25, 2025
  • KIKAO KAZI CHA WENYEVYITI WA BODI NA WATENDAJI WAKUU WA TAASISI ZA UMMA (CEOs Forum 2025)

    August 24, 2025
  • Tazama zote

Video

Video zaidi

Viunganishi vinavyoingiliana

  • Leseni ya vileo
  • Fomu ya ukaguzi

Viunganishi vinavyohusiana

  • Tovuti kuu ya serikali
  • Tamisemi
  • Utumishi portal
  • Wakala wa serikali mtandao
  • Mkoa wa arusha
  • ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Sekei Road

    Anuani ya posta: 2330 Arusha

    Simu : +255 027 2502737

    Simu: 073 65000476

    Barua pepe: ded@arushadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.