• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe |
Arusha District Council
Arusha District Council

Serikali ya jamuhuri ya Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili Makuu
    • Mikkati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara na Vitengo
      • Utawala na Utumishi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Fadha na Biashara
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliji
      • Ardhi na Maliasili
      • Maji
      • Works
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo na Umwagiliaji na Ushirika
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Internal Audit
      • Nyuki
      • Uchaguzi
      • UKIMWI/ AIDS
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Livestock
    • Wadau wa Maendeleo
  • Huduma Zetu
    • Health
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Utawala Fedha na Mipango
      • Elimu Afya na Maji
      • Kudhibiti UKIMWI
      • Maadili ya Madiwani
      • Uchumi Ujenzi na Mazingira
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Vikao vya Timu ya Uendeshji ya Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mktaba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa UMMA
    • Video za Shoghuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

BALOZI WA JAPAN NCHINI AMEKABIDHI MTAMBO WA KICHUJIA MAJI KUONDOA MADINI YA FLORAIDE KIJIJI CHA LEMANDA

Posted on: January 28th, 2023

Serikali ya Japan kupitia ubalozi wake nchini Tanzania, umekabidhi msaada wa mtambo maalum wa kuchujia maji na kuondoa madini hatari ya floraidi, kwa wananchi wa kijiji cha Lemanda kata ya Oldonyosambu.

Akizungumza wakati wa hafla ya kuzindua na kukabidhi mradi huo iliyofanyika kijijini hapo, mgeni rasmi na Balozi wa Japan nchini Tanzania Yashushi Misawa, amesema kuwa serikali ya Japan imefikia hatua hiyo mara baada ya kutambua kiasi kikubwa cha floraidi kwenye maji ya eneo hilo na kkuon madhara wanayoyapata watu wanaotumia maji hayo.

"Tafiti zinaonesha maji ya eneo hili yanamadini ya frolaidi yaliyozidi mm 24 kwa lita, ambayo yana madhara makubwa kwa binadamu, mtambo huu utaondoa madini hayo na kufikia  mm 0.1 kwa lita kiasi kinachokubalika kimataifa kwa matumizi ya binadamu" Amebainisha Balozi Misawa.

Aidha Balozi huyo ameweka wazi kuwa, uwepo wa mtambo huo, utasaidia kuondoa changamoto kwa watoto wanaozaliwa sasa na kuwataka wananchi hao kuhakikisha wanatumia maji hayo kwa matumizi ya nyumbani kwa kunywa na kupikia.

Katibu Tawala wilaya ya Arumeru, Mwl. James Mchembe, amesema kuwa serikali inatambua na kuthamini juhudi za serikali ya  Japan kwa watanzanzia, na inaahidi kuendelea kuweka mazingira rafiki ili kudumisha ushirikiano huo kwa lengo la kutatua changamoto za kijamii nchini.  

Nao viongozi wawakilishi wa wananchi  licha ya kuushukuru ubalozi wa Japan, wamethibitisha kuwepo madhara makubwa kwa watu kutokana na kutumia maji yenye floraidi iliyozidi na kuahidi kuutunza mtambo pamoja na kuhakikisha matumizi sahihi ya maji hayo hususani kwa watoto.

Mwenyekiti wa halmashauri ya Arusha, Mhe. Ojung'u Salekwa amebainisha kuwa, mtambo huo ni neema ya kipekee iliyowashukia wananchi wa Lemanda na kuuomba ubalozi huo kuona umuhimu wa kuongeza mtambo ambao utawafikiwa wananchi wa vitongoji vyote vitatu vyenye changamoto kama hiyo.

"Tunashukuru kwa mtambo huu, Mhe. Balozi kama unavyoshuhudia watoto wetu wamepinda miguu na wengine kuwa na vichwa vikubwa, tukuombe mtusaidi kupata mtambo mwingine utakaowasaidia wananchi wa vitongoji vingine viwili vya kijiji hiki".Amesisitiza Mhe. Raymond Lairumbe, Diwani  wa kata ya Oldonyowas

Akisoma risala kwa niaba ya wananchi wa Lemanda Afisa Mtendaji wa Kata, Lomunyaki Ndiyogi amebainisha uwepo wa changamoto ya watoto walioathitika na madini ya floraidi kushindwa kutembe na kufika shule hivyo kuiomba serikali ya Japan kujenga madarasa ya awali kwenye kitongoji  cha Ngivilati ili watoto hao waweze kusoma ndani ya kitongoji chao.

Mtambo huo wa kuchuja maji  umetengenezwa na chuo kikuu cha Shunshi cha nchini Japan, una uwezo wa kuzalisha Lita 300 kwa saa na kuhudumia jumla ya 60 na watu zaidi ya 400 wa kitongoji cha Lemanda, umegharimu dola za kimarekani 115,000 sawa na shilingi milioni 264 za kitanzania.


"ARUSHA DC Yetu, Tushirikiane Kuijenga"

#kaziinaendelea✍














Matangazo

  • KUITWA KWENYE USAHILI WA NAFASI ZA UDEREVA TAREHE 28/12/2018 December 19, 2018
  • MAADHIMISHO YA WIKI YA UNYONYESHAJI DUNIANI TAREHE 1-7, AGOSTI 2020. July 31, 2020
  • TANGAZO KWA WANANCHI WOTE MKUTANO WA BARAZA LA MADIWANI WA ROBO YA PILI 2O20/2021 TAREHE 29.01.2021 January 29, 2021
  • KINGA TIBA YA KICHOCHO NA MINYOO YA TUMBO KWA WATOTO MIAKA 5-14 March 02, 2021
  • Tazama zote

Habari mpya

  • DC ARUMERU ATEMBELEA MAENEO YALIYOPATA MADHARA YA MVUA ARUSHA DC..

    March 24, 2023
  • MVUA KUBWA YALETA MADHARA ARAFA YA MUKULAY ARUSHA DCA DC

    March 24, 2023
  • MVUA KUBWA YALETA MADHARA ARAFA YA MUKULAT ARUSHA DC

    March 24, 2023
  • DC ARUMERU AFANIKISHA MCHANGO WA MAZIWA YA MTOTO KWA KAYA ILIYOBOMOKEWA NYUMBA OLMOTONY

    March 24, 2023
  • Tazama zote

Video

MFUGAJI AKIELEZEA FAIDA ZA UHIMILISHAJI WA NG'OMBE WA MAZIWA - BANDA LA MIFUGO ARUSHA DC
Video zaidi

Viunganishi vinavyoingiliana

  • Leseni ya vileo
  • Fomu ya ukaguzi

Viunganishi vinavyohusiana

  • Tovuti kuu ya serikali
  • Tamisemi
  • Utumishi portal
  • Wakala wa serikali mtandao
  • Mkoa wa arusha
  • ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Sekei Road

    Anuani ya posta: 2330 Arusha

    Simu : +255 027 2502737

    Simu: 073 65000476

    Barua pepe: ded@arushadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.