Na Elinipa Lupembe
Balozi wa Japan nchini Tanzania Mheshimiwa Balozi Yashushi Misawa, akiwatwisha ndoo ya maji kinamama Nawisa Sareyo na Ngaleiyai Saimali wakazi wa kijiji cha Lemanda mara baad aya kuzindua mradi wa maji kijijini hapo.
Serikali ya Japan kwa kushirikiana na Serikali ya Tanzania imetengenza mtambo wa kuchujia maji ili kuondoa taka hususani madini hatari ya floraidi.
Mtambo huo wa kuchuja maji wenye uwezo wa kuzalisha Lita 300 kwa saa na kuhudumia jumla ya 60 na watu zaidi ya 400 wa kitongoji cha Lemanda na umegharimu dola za kimarekani 115,000 sawa na shilingi milioni 264 za kitanzania.
Wananchi wa Lemanda wameushukuru ubalozi wa Japani kwa msaada huo, ambao wanaamini utakwenda kupunguza madhara wanayoyapata kutokana matumizi ya maji yenye kiasi kikubwa cha madini ya floraidi.
ARUSHA DC Yetu, Tushirikiane Kuijenga"
#KaziInaendelea✍✍✍
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.