Wajumbe wa Baraza la Madiwani Halmashauri ya Wilaya ya Arusha kwa pamoja wameazimia kuipitisha bajeti ya Halmashauri hiyo kiasi cha shilingi bilioni 71 kwa mwaka wa fedha 2025/2026.
Makamu Mwenyekiti Halmashauri ya Wilaya ya Arusha Mh.Fredy Lukumay amewapongeza wajumbe wa Baraza Hilo kwa kuazimia kupitishwa kwa bajeti hiyo,huku akitoa shukrani za dhati kwa idara ya mipango na uratibu kwa kazi nzuri waliyoifanya ya kuandaa bajeti hiyo.
"Kwakweli niseme tu tumeridhishwa na bajeti hii,nichukue nafasi hii kuipongeza Idara ya mipango Halmashauri ya Wilaya Arusha kwa kuandaa bajeti nzuri na yenye tija kwa wananchi wetu". Alisema Mh.Fredy
Vile vile, Mh Fredy aliongeza kwa kusema kuwa bajeti iliyopitishwa imezingatia maelekezo ya Serikali sambamba na utekelezaji wa Irani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwani imejikita katika kutekeleza miradi ya maendeleo ya Wananchi.
"Bajeti hii imegusa maeneo muhimu ikiwemo afya, Elimu,miundombinu katika kuzingatia maboresho na utengenezaji wa barabara kwa kata zote 27,kwa ujumla sisi Madiwani kwaniaba ya wananchi tumeridhika na bajeti hii, tunachotarajia sasa ni bajeti hii iweze kupitishwa dodoma kwa ajili ya utekelezaji".Alisema Mh Fredy.
Kwa upande wake Mh.Eric Semboja Diwani Kata ya Olorien alisema kuwa bajeti iliyopitishwa inatarajiwa kukamilisha baadhi ya miradi ambayo haikukamilika kwa mwaka wa fedha 2024/2025, hivyo bajeti hiyo itakwenda kukamilisha miradi miradi hiyo sambamba na ikiwemo kutekeleza miradi mingine mipya kwenye Kata zote 27.
"Kwakweli tunarajia kuona mabadiliko mengine makubwa kupitia bajeti hii,pamoja na kukamilisha baadhi ya miradi ambayo bado iko kwenye utekelezaji lakini wananchi watarajie kuona miradi mingine mipya na yenye tija kwenye maeneo yao ambayo itasaidia kuchochea uchumi kwa vijana wetu". Alisema Mh.Eric.
Baraza hili maalum la madiwani limekutana kwa ajili ya kupitisha bajeti ya mwaka wa fedha 2025/2026,likiwa limeudhuliwa pia na Taasisi nyinginezo za Serikali ikiwemo Tarura,Ruwasa,Tanesco pamoja wataalam wa idara mbalimbali kwa ajili ya kuwakilisha mipango yao ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha ikiwa ni utaratibu wa baraza hilo katika kuwahusisha wakuu
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.