BARAZA LA MADIWANI HALMASHAURI YA WILAYA YA ARUSHA LAMPONGEZA RAIS DKT.SAMIA KWA KUPELEKA FEDHA NYINGI KWENYE MIRADI YA MAENDELEO KATIKA HALMASHAURI HIYO.
Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha wamshukuru na kumpongeza Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuiletea Halmashauri hiyo fedha nyingi kwa ajili ya miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo sekta ya Afya,Maji,Elimu pamoja na kurejesha mikopo ya 10% kwa Wanawake,Vijana na Watu wenye Ulemavu.
Pongezi hizo zimetolewa na Mhe. Freddy Lukumay Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo wakati akifungua kikao cha Baraza la Madiwani ambapo amesema Halmshauri hiyo ina Kata 27,na katika kila Kata kuna miradi ya ujenzi wa Shule, Zahanati na Vituo vya Afya, Miradi ya Maji, sambamba na Vikundi vilivyonufaika na mikopo ya 10%,huku asilimia kubwa ya fedha hizo ni kutoka Serikali Kuu
Sambamba na hilo, Makamu Mwenyekiti huyo ametoa pongezi kwa ushirikiano ulipo katika ya Waheshimiwa Madiwani na Wataalamu ambapo amesema umepelekea Halmashauri hiyo kufanya vizuri katika ukamilishwaji wa miradi yake kwa wakati na kwa ubora na kwa kuonyesha thamani halisi ya fedha zilizotumika katika utekelezaji wa miradi hiyo.
Kikao hicho pamoja na mambo mengine kiliweza kupokea na kujadili taarifa mbali mbali ikiwemo Kamati ya Utawala na Mipango, Kamati ya Kudhibiti UKIMWI, Mradi wa Redio ya Halmashauri,Kamati ya Elimu na Afya, Kamati ya uchumi, Ujenzi na Mazingira pamoja na Taarifa ya utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo robo ya pili Kwa mwaka wa fedha 2024/2025 .
Mbali na hayo,Baraza hilo pia limewataka Watumishi wa Halmshauri hiyo kuendelea na moyo wa kujituma katika kusimamia shughuli za kila siku za Halmashauri hiyo hususan katika kuwahudumia wananchi pamoja na usimamizi mzuri wa miradi ya maendeleo kwa wanachi kwani Serikali imekuwa ikitoa fedha nyingi kwenda kwenye Kata na Vijiji mahali ambako jamii inaishi.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya hiyo Ndg, Seleman H. Msumi amewashukuru wajumbe wa Baraza la Madiwani na kuendelea kusisitiza kuwa yeye na timu ya Watalaam wataendelea kushirikiana na Waheshimiwa Madiwani hususan katika kusimamia miradi ya maendeleo inayotekelezwa katika Kata zao.

Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.