Na. Elinipa Lupembe.
Wajumbe wa Baraza la Madiwani halmashauri ya Arusha, wilaya ya Arumeru, waimeshauri Serikali kuangaliwa upya mwenendo wa Kamati za usimamizi wa miradi inayotekelezwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii - TASAF, kwa kuwa baadhi ya miongozo imekuwa hazitoi fursa kwa viongozi wa ngazi ya kata kuwajibika kwenye kamati hizo.
Akizungumza wakati wa mkutano wa Baraza la Madiwani, Diwani wa Viti Maalum, mheshimiwa Jasmin Bachu, amesema kuwa, baadhi ya wajumbe wa kamati hizo, wameonekana kutokuwa waaminifu na kushindwa kuwajibika ipasavyo katika katika usimamizi wa miradi ya maendeleo na viongozi wa kata kushindwa kukemea ja,bo hilo, kutokana na viongozi hao, kutokuwa na uwezo wa kufanya hivyo kisheria.
Licha ya kuzungumza hayo, Mhe. Bachu amesema kutokana na sheria, kanuni na miongozo iliyopo kwa sasa, inawanyima nafasi hata madiwa kuhoji na kupata taarifa za wazi az shughuli zote za maendeleo zinazosimamiwa na kamati hizo.
Aidha wameishauri serikali, kufanyike marekebisho kwenye miongozo ya TASAF, juu ya uundwaji wa kamati hizo, ziweze kuwajibika kwa viongozi wa kuanzika ngazi ya kijiji, kata na halmashauri, ili usimamizi wa miradi hiyo ufanyike kwa uwazi kwa wananchi wote.
"Kutokana na kamati hizo, kutowajibika moja kwa moja kwa viongozi wa ngazi ya kata, kumekuwa na ukosefu wa taarifa za wazi za utekelezaji wa miradi hiyo kwa wananchi na kuwafanya madiwani kushindwa kuhoji hata wanapoona mapungufu" amesema Diwani huyo.
Naye Mwenyekiti wa halmashauri ya Arusha, Baraka Simon, amekitaka Kitengo cha TASAF, kukusanya maoni yote na kutuma mapendekezo kwa Serikali kuu, ili kufanya marekebisho, baadhi ya kanuni na taratibu ambazo zitatoa fursa kwa viongozi wa kata kuhusika moja kwa moja kwenye usimamizi wa miradi ya maendeleo katika jamii.
"Mratibu wa TASAF, kusanya maoni ya wajumbe na kutuma mapendekezo hayo kwa serikali kuu kwa lengo la kuboresha baadhi ya sheria ambazo haziwaruhusu Madiwani, kuingia moja kwa moja kusimamia miradi ya TASAF tofauti na kuizungumzia kwenye mikutano ya Baraza" amesema Mwenyekiti.
Hata hivyo Mratibu wa TASAF, Grace Makema ameafiki kuwasilisha mapendekezo hayo serikali kuu, na kutoa ufafanuzi wa miundo ya kamati za miradi ambayo inatolewa na serikali kuu ikiwa ni lengo halisi la miradi ya jamii kusimamiwa na jamii yenyewe.
Amefafanua kuwa, Wajumbe wa Kamati hizo, huchaguliwa na wananchi kwenye mkutano mkuu wa kijiji, na kupewa mafunzo ya kuwajengea uwezo wa usimamizi wa miradi na zinawajibika kwa viongozi wa serikali ya kijiji, licha ya kukumbana na baadhi ya changamoto za kimahusiano kati ya viongozi wa vijiji na viongozi wa kata, wakiwemo maofisa watendaji wa kata na waheshimiwa madiwani.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.