• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe |
Arusha District Council
Arusha District Council

Serikali ya jamuhuri ya Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili Makuu
    • Mikkati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara na Vitengo
      • Utawala na Utumishi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Fadha na Biashara
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliji
      • Ardhi na Maliasili
      • Maji
      • Works
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo na Umwagiliaji na Ushirika
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Internal Audit
      • Nyuki
      • Uchaguzi
      • UKIMWI/ AIDS
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Livestock
    • Wadau wa Maendeleo
  • Huduma Zetu
    • Health
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Utawala Fedha na Mipango
      • Elimu Afya na Maji
      • Kudhibiti UKIMWI
      • Maadili ya Madiwani
      • Uchumi Ujenzi na Mazingira
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Vikao vya Timu ya Uendeshji ya Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mktaba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa UMMA
    • Video za Shoghuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

Wakazi wa Bwawani wapata huduma ya kupima afya bure

Posted on: July 19th, 2018

Na. Elinipa Lupembe

Wananchi wa kata ya Bwawani na vitongoji vyake, wamejitokeza kwa wingi kuchangamkia huduma ya kupima afya bure, iliyotolewa kwenye Zahanati zao kwa siku tatu mfululizo,  huduma iliyotolewa bure bila malipo yoyote.

Huduma hiyo ya vipimo na dawa imetolewa  na halmashauri ya Arusha kwa ufadhili wa wadau wa afya kutoka Shirika la Project Abroad - Tanzania, ambapo watu wamepata fursa ya kupima afya zao na kupatiwa dawa mara baada ya ugonjwa kugundulika.

Wananchi hao,  licha ya kushangazwa na huduma hiyo, ambayo haijawahi kutokea ndani ya kata yao,  wamesema kuwa wamepata fursa ya kuchunguza afya zao kwa magonjwa mbalimbali ambayo hawakuwahi kufikiria kupima bila ya kuugua.

Mwenyekiti wa kijiji cha Mungushi, mheshimiwa Jacob Toronge, amesema kuwa, kutokana kata hiyo kuwa pembezoni mwa mji, sio rahisi mtu kwenda hospitali kupima bila ya kuwa mgonjwa, kutokana na umbali wa eneo loa mpaka kufika hospitali.  

Toronge ameongeza kuwa kituo cha Afya kipo Nduruma zaidi ya Kimita 15 huku hospitali ya mkoa ni zaidi ya Kilomita 30, hivyo sio rahisi sana mtu, kutoka Bwawani kwenda hospitalikupima bila kuugua.

"Tunaishi mbali sana na hospitali na vituo vya afya,  mtu wa Bwawani ni vigumu kwenda hospitali bila kuugua, ni mpaka awe mgonjwa ndipo anaweza kwenda hospitali, lakini leo tumerahisishiwa kwa kuletewa huduma za vipimo nyumbani" amesema Mwenyekiti huyo.

Mchungaji  Julius Loita, aliyefika kupima afya, kwenye moja ya zahanati kupata vipimo, amesema kuwa, huduma ya upimaji afya ni ya msingi kwa wananchi hasa, waishio maeneo ya pembezoni, kwa kuwa inawapa fursa kujua hali za afya zao.  

Mkurugenzi wa mradi,  shirika la Project Abroad  Florence Mdodi, amesema kuwa shirika lao linajishughulisha na uchunguzi, wa hali ya afya kwa jamii, kwa kutoa fursa ya watu kupima magonjwa yasiyoambukiza na yanayoambukiza pamoja na kutoa dawa za magonjwa hayo.

Aidha Mdodi, amefafanua kuwa, lengo la kutoa huduma hiyo ni kuwataka watu kupima afya zao, hata kama hawajisikii kuumwa kitu chochote kutokana na ukweli kuwa, kuna baadhi ya magonjwa huchelewa kuonesha dalili.

"Ni utaratibu mzuri kwa mtu, kuwa na tabia ya kufanya uchunguzi wa afya mara kwa mara  ili kuepuka madhara ya kuachelewa kuanza matibabu" amesisitiza Mdodi.

Ameongeza kuwa, ugonjwa wowote ukigundukika mapema ni rahisi kutibika na mgonjwa kurudia afya yake haraka,  tofauti na ugonjwa ukigundulika kwa kuchelewa mgonjwa anaweza kupoteza maisha.  

Naye Muuguzi Mkuu, halmashauri ya Arusha sista Agusta Komba ameyataja magonjwa yaliyokuwa yanapimwa ni pamoja na ugonjwa wa macho, pressure, magonjwa ya mfumo wa hewa, maambukizi ya njia ya mkojo 'UTI', Vidonda vya tumbo na minyoo pamoja na HIV.

Hata hivyo, Muuguzi huyo amesema kuwa, watu waliogundulika na magonjwa walipatiwa ushauri nasaha pamoja na dawa na wale waliokutwa hawana ugonjwa wowote walipatiwa ushauri wa namna ya kuendelea kujikinga kupata magonjwa.

Ameongeza kuwa na baadhi ya wagonjwa, walipatiwa rufaa kwenda hospitali za wilaya na mkoa kwa matibabu na uchunguzi zaidi.

Aidha, Komba amesema kuwa zaidi ya wananchi mia nane, wamejitokeza na kupata huduma za vipimo na  kupatiwa dawa huku akisisitiza kuwa huduma hiyo itakuwa inatolewa kila baada ya miezi minne kwenye, maeneo ya pembezoni ambako hakuna vituo vya afya vyenye maabara.  

Huduma hiyo imetolewa kwenye zahanati za Themiyasimba, Mungushi, Bwawani pamoja na zahanati ya Kyoga kata Olturoto.

Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA MKATABA ENABOISHU FM - ARUSHA DC May 26, 2025
  • ORODHA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO 2023 ARUSHA DC June 11, 2023
  • ZIARA YA WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS TAMISEMI, MHE. MOHAMED O. MCHENGERWA 17 SEPTEMBA 2024 September 13, 2024
  • MTIHANI WA DARASA LA SABA 11-12/09/2024 September 09, 2024
  • Tazama zote

Habari mpya

  • VIONGOZI WA DINI WAPEWA ELIMU YA CHAKULA BORA

    May 28, 2025
  • VIONGOZI WA DINI WAPEWA ELIMU YA AFYA YA MAMA NA MTOTO

    May 27, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA MKATABA

    May 26, 2025
  • RC MAKONDA ATEMBELEA NA KUKAGUA MRADI WA UJENZI WA MAHAKAMA YA AFRIKA ARUSHA

    May 25, 2025
  • Tazama zote

Video

Video zaidi

Viunganishi vinavyoingiliana

  • Leseni ya vileo
  • Fomu ya ukaguzi

Viunganishi vinavyohusiana

  • Tovuti kuu ya serikali
  • Tamisemi
  • Utumishi portal
  • Wakala wa serikali mtandao
  • Mkoa wa arusha
  • ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Sekei Road

    Anuani ya posta: 2330 Arusha

    Simu : +255 027 2502737

    Simu: 073 65000476

    Barua pepe: ded@arushadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.