Na. Elinipa Lupembe.
Uongozi wa halmashauri ya Arusha, umetakiwa kuanza kuandaa mpango wa matumizi ya maeneo yote ya umma 'site plan' ili kuwa na mpango bora wa matumizi bora ya maeneo hayo kwa sasa na miaka ijayo.
Rai hiyo imetolewa na Wajumbe wa kamati ya Siasa wilaya ya Arumeru, wakati wa kikao cha majumuisho ya ziara ya siku mbili ya kukagua utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika halmashauri ya Arusha, kikao kilichofanyika kwenye ukumbi wa mwenyekiti wa halmashauri hiyo.
Wajumbe hao waketoa agizo hiloo baada ya kujionea ongezekomlamlasi la ujenzi wa majengo yanayojengwa katika maeneo ya shule za msingi na sekondari, majengo ambayo yanadhihirisha wazi kuwa kukosekana kwa mpango wa matumizi, kutasababisha kuwa na majengo yasiyo n mopangilio katika maeneo hayo ya Umma.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi, mheshimwa Simon Ole Saning'o amesema kuwa ni vyema halmashauri ikaanza utaratibu wa kuandaa mpango wa matumizi ya maeneo 'site plan', katika maeneo yote ya umma ikiwemo shule, hospitali, vituo vya afya na zahaanati, lengo likiwa ni kuwa na majengo ambayo yamepangwa katika eneo husika.
"Serikali inatoa pesa za kujenga miundombinu katika ssekta za elimu na afya, kutokana na kasi ujenzi wa majengo, anzeni kuwa na 'site plan' za maeneo hayo ili kuondoa hali ya majengo holelaa yasio na mpangilo, kkama ni eneo la shule kuwe na plan inayoonyesha eneo la madarasa, vyoo, nyumba za walimu, viwanja na sio kuwa na majengo holela'amesisitiza Mwenyekiti huyo wa CCM Arumeru.
Hata hivyo Maenyeki huyo amesema kuwa uwepo wa mpago wa matumizi ya maeneo ya umma uende sambamba na ujenzi wa majengo ya magorofa, ujenzi ambao utazingatia ufinyu wa ardhi katika halamshauri yaArusha, na kuongeza kuwa, uwepo wa majengo yaliyo kwenye mpangilio mzuri katika maeneo ya Umma, licha ya kuwa na muonekano mzuri lakini pia utachangia matumizi bora ya arddhi.
Aidha mheshimwa Saning'o, ameishukuru serikali ya awamu ya sita kwa kutoa pesa kwa ajili ya kuteleleza miradi mbalimbali kisekta, miradi ambayo inadhihirisha utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapiinduzi iliyonadiwa wakati wa uchaguzi mkuu wa mwaka 2020.Aidha amewataka wananchi wa Arumeru, kuendelea kuunga mkono juhudi za serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Mheshimiwa mama Samia Suluhu Hassan kwa kuifanya kazi kwa bidii huku waakilinda amani iliyopi kwa maendeleo ya taifa la Tanzania.
Hata hivyo Mwenyekiti wa halmashauri ya Arusha, mheshimiwa Ojung'u Salekwa licha ya kuishukuru Kamati ya Siasa kutembelea na kukagua shughuli za utekelezaji wa miradi ya maendeleo inahotekelezwa katika halamshauri hiyo, amesema kuwa halamshauri imepokea maelekezo hayo na kuanza kuyafanyia kazi kwa haraka na kuongeza kuwa tayari halamshauri imeanza kuandaa mipango ya matumiza ya maeneo ya umma 'site plan' na wanaendelea kukamilisha maeneo ambayo bado.
Awali Kamati ya siasa wilaya ya Arumeru, imefanya ziara ya kukagua jumla ya miradi 12 yenye thamaniya shilingi milioni 637, fedha zilizotolewa na serikali kuu, ziara yenye lengo la kufuatailia utkelezaji wa Ilaani ya Chama cha Mapinduzi ya mwaka 2020 -2025.
ARUSHA DC
KAZI IENDELEE✍
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi wilaya ya Aruemeru Mhe. Simon Ole Saning'o akizungumza kwenye kikao cha majuisho, baada ya ziara ya Kamati ya Siasa wilaya ya Arumeru kukagua miradi ya maenedleo halmashauri ya Arusha, kwenye ukumbi wa mikutano wa Mwenyekiti wa halamshauri hiyo.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.