Mkurugenzi Mtendaji, halmashauri ya Arusha, Seleman Msumi, anawatangazia Wazazi na Walezi wote, wenye watoto wenye umri wa kuanzia miaka 0 - 5, kuwapeleka watoto wao kupata Chanjo ya Polio.
Chanjo hiyo ya Polio itatolewa kwa siku nne, kuanzia tarehe 28.04 hadi 01.05, 2022 kwenye Vituo vyote vya Kutolea huduma za Afya vya halmashauri ya Arusha.
Vituo vyote vya kutolea Huduma za Afya, vitafunguliwa na kufanya kazi kuanzia saa 02:00 Asubuhi mpaka saa 12:00 Jioni.
EWE MZAZI/MLEZI MKINGE MWANAO DHIDI YA UGONJWA WA POLIO, CHANJO INAYOTOLEWA BURE NA SERIKALI
"KINGA NI BORA KULIKO TIBA"
ARUSHA DC
KaziInaendelea✍✍
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.