Mkurugenzi Mtendaji, halmashauri ya Arusha, Seleman Msumi, anawatangazia Wazazi na Walezi wote, wenye watoto wenye umri wa kuanzia miaka 0 - 5, kuwapeleka watoto wao kupata Chanjo ya Polio.
Chanjo hiyo ya Polio itatolewa bure kwa muda wa siku nne, kuanzia tarehe 01 - 04 Septemba, 2022 kwenye Vituo vyote vya Kutolea huduma za Afya vya ndani ya halmashauri ya Arusha.
Vituo vyote vitafunguliwa na kufanya kazi kuanzia saa 02:00 Asubuhi mpaka saa 12:00 Jioni.
EWE MZAZI/MLEZI MKINGE MWANAO DHIDI YA UGONJWA HATARI WA POLIO, CHANJO INAYOTOLEWA BURE NA SERIKALI
'Mpe Matone....., Okoa Maisha'
"KINGA NI BORA KULIKO TIBA"
Ukisoma tangazao hili, mjulishe na mwingine!!!
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.